Monday, June 27, 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE AZINDUA STUDIO YA REDIO YA JAMII KATIKA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA.

N5Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda kwenda kuzindua Studio ndani ya Chuo hicho 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
N3Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
N1Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa toka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa Uzinduzi wa ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
N2Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
N4Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amezindua studio ya redio ya jamii ya ‘Community Media Network of Tanzania’ (COMNET)   katika Chuo kuku Huria( OUT )  itakayotumika kusambaza habari maeneo yenye uhaba wa redio.
Uzinduzi huo umefanyika   leo jijini Dar es Salaam,ambapo Mhe. Waziri  amesema kuwa studio hiyo itasaidia  idadi kubwa ya wanachi wanaoishi vijijini kupata habari kutoka Serikalini na kutoa mrejesho wa kile watakachosikia kwa urahisi.
“Ni Studio muhimu kwa ajili ya kusambaza demokrasia  kwa watu hasa wale waliopo vijijini kwa vile redio nyingi bado hazijawafikia”Alisema Mhe.Nape.
Aidha amewataka wanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari na  mawasiliano kwa umma katika  chuo  hicho kutumia studio hiyo kujifunza zaidi kwa vitendo na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye ukweli kutoka vyanzo sahihi ili kutoa ujumbe wenye manufaa mazuri kwa jamii.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda amesema studio hiyo imeanzishwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO)  kwa lengo kutoa elimu kwa jamii ambayo imekuwa haipati habari kwa urahisi.
Amewataka wanahabari na wananchi kwa ujumla   kufikisha habari katika studio hizo kwa kuwa inatumia njia ya haraka na rahisi katika kufikisha ujumbe kwa kushirikiana na redio mbalimbali za jamii.
 Naye mwakilishi kutoka Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi,na Utamaduni(UNESCO) Bi. Zulimira Rodrigues  amesema studio ya redio ya ‘Community’ ipo kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo ya wanawake na vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mpaka sasa Shirika hilo limefanikiwa kuanzisha redio za jamii katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara ambayo ni Mwanza,Arusha na Tanga na katika baadhi ya maeneo ya Unguja na Pemba.

No comments: