Sunday, June 12, 2016

ZITTO azidi kuandamwa,Kongamano la ACT lapigwa stop,Polisi watanda Ukumbini,hakuna kuingia

Mama ANNA MGWIRA mwenyekiti wa chama hicho akizungumza na wanahabari dakika chache zilizopita katika ofisi za makao makuu ya chama hicho
Kongamano lililokuwa limeandaliwa na cham cha kisiasa cha ACT WAZALENDO chini ya kiongozi wake mkuu ZITTO KABWE limeshinda kufanyika baada ya watu wanaodhaniwa ni polisi kuzuia kongamano hili bila kutoa sababu yoyote kwa wandaaji hao.

Kongamano hilo ambalo lilitakiwa kuanza leo siku ya juumapili saa saba mchana katika ukumbi wa LAPF millennium Tower Dar es salaam limeshindwa kufanyika kutokana na Askari waliokuwa wametanda nje ya ukumbi huo wakiwazuia wanachama na wadau mbalimbali waliokuwa wamealikwa katika kongamano hilo.

Akizungmza na wanajanari muda mfupi baada ya Kuzuiwa kwa kongamano hilo mwenyekiti wa ACT WAZALENDO Mama ANNA MGWIRA amesema kuwa taarifa za kuziuwa kwao wamezipata kutoka kwa mmiliki wa ukumbi huo ambapo amewaambia kuwa Wamepigiwa simu na askari kuwa wasiruhusu kufanyika kwa kongamano hilo kinyume na hivyo wangefungiwa biashara yao hiyo.

Ameendelea kusema kuwa waliambiwa na mmiliki wa ukumbi huo kuwa askari walianza kutanda nje ya ukumbi huo tangu saa 12 asubuhi jambo lililoashiria kuwa kongamano hilo halitafanyika.

MGWIRA amesema kuwa wao kama chama wameshtushwa sana na taarifa hizo ambazo hata walipompigia kamanda wa polisi mkoa amesema kuwa hana taarifa za kuzuiwa kwa kongamano hilo jambo ambalo linawapa mashaka kuwa ni nani anafanya mambo hayo ambayo yanarudisha nyuma democrasia.

Baada ya kuzuiwa sasa chama hicho kimetangaza kuwa kitakutana kwa dharura na kujadili hali inayokikumba chama hicho ikiwa ni wiki mojua tuu kwa kiongozi wao ZITTO KABWE kuhojiwa na njeshi la polisi kuhusu kauli zake juu ya Rais katika mkutano wake wa mbagala.

Kongamano hilo awali lilielezwa kuwa ni kwa ajili ya kujadili maswala muuuhimu ya Bajeti na kumpa nafasi kiongozi wao huyo kutoa maoni yake juu ya bajeti ya mwaka huu kwa kuwa  hawezi kuyatoa bungeni kutokana na kusimamishwa kwake kuhudhuria vikao vya bunge

No comments: