Monday, July 4, 2016

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO, MILVIK KUSHIRIKIANA KUTOA BIMA WATAKAYOIMUDU WATANZANIA

 Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitangaza ushirikiano kati yao na Tigo kutoa bima watakayoimudu watanzania. Kutoka kushoto ni Meneja wa Promosheni wa Tigo, Mary Rutta, Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel na Meneja Maendeleo ya Biashara wa Resolution Insurance, Zamaradi Mbega.
  Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (wa pili kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Meneja wa Promosheni wa Tigo, Mary Rutta akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu bima hiyo.
 Meneja Maendeleo ya Biashara wa Resolution Insurance, Zamaradi Mbega (kulia), akizungumzia mpango huo wa bima.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania itashirikiana na na Milviki Tanzania  na kampuni ya bima ya Resolution kuanzisha huduma  mpaya ya Bima iliyoboreshwa  ikijulikana Bima Mkononi. Tigo imekuwa ikitoa huduma  kama hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita  kwa wateja wake zaidi ya 500,000 kupitia Tigo Bima.Huduma ya Bima Mkononi inatoka huduma ya kipekee  kama vile bima ya maisha, ugonjwana ajali kwa mtu binafsi kwawateja ambao wanaotumia huduma ya Tigo Pesa.

Akitangaza kuzinduliwa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin alisema, “Huduma hii itasaidia kuziba pengo  kati ya wateja  na hivyo kuongeza  upenyezaji wa huduma hiyo kwa njia ya simu katika maeneo ya mjini na vijijini nchini Tanzania, tunaamini Bima Mkononi  itakuwa ni kicdhocheo kikubwa  cha kusukuma ujumuishwaji wa  huduma za fedha  katika sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania kuzifikia huduma za bima  wanazozimudu kutoka kwenye simu zao.” 

Chaplain aliongeza, “Tunawaomba Watanzania  ambao  hawajaweza kuzifikia  huduma za afya ambao wanazimudu  ao  bima ya kawaida ya afya  kuanza kutumia huduma hii  kwa sababu  inatoa ulinzi dhidi ya majanga ya kifedha  na afya duni kwao na familia zao.” 

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Kuzinduliwa kwa huduma hii  kupo kwenye mikakati ya Tigo ya kuboresha mageuzo katika mfumo wa maisha ya kidijitali na katika kuongoza kwake  katika kutoa teknolojia ya kisasa  na ubunifu  kwa kuwezesha huduma ya Bima Mkononi kufikiwa kupitia Tigo Pesa.”

Aliongeza, “Huduma hii mpya  itakuwa ni fursa kubwa kwa wateja wa Tigo  kuipata huduma ya bima kwa urahisi  kwa sababu huduma ya Bima Mkononi  inalenga kuwapatia Watanzania  njia mbadala  kwa bima za afya na maisha.”

Aliipongeza Milvik  kwa ushirikiano wake  na kuahidi kuwa Tigo imelenga  kuendelsa  kuunga mkono  kupitia huduma ya Tigo Pesa.
Hivi karibuni Tigo ilizindua  kampeni mpya   ya NITIGOPESA ambapo wateja kutoka mitandao yote  ya simu  wanaweza kupata huduma za  kifedha kutoka kwa wateja na wafanyabiashara kote nchini.

No comments: