NYINGINE YA KUPENDEZA--WANANCHI WA WILAYA YA UBUNGO WAKO MBIONI KUSOGEZEWA HUDUMA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob akisalimiana na Mkuu wa Wialaya ya Ubungo Mhe. Humphrey Polepole alipokaribishwa katika Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam. Polepole amekaribishwa ili apate fursa ya kutambulishwa kwa Madiwani ambao kwa namna moja au nyingine atakuwa akifanya kazi nao kwa kuwa Wilaya yake imetokana na Manispaa hiyo.
Frank Shija,MAELEZO
Mchakato wa kukamilisha taratibu za kuanza rasmi kwa shughuli za kiutendaji kwa Ofisi za Mkuu wa wilaya na Manispaa ya Ubongo uhuko mbio kukamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ubungo Mhe. Boniface Jacob wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani leo jijini Dar es Salaam. Mhe. Jacob amesema kuwa amearifiwa kuwa taratibu za kugawa rasilimali zimekamilika kinachosubiriwa tu ni kukamilika kwa suala la upatikanaji wa majengo ya Ofisi ambayo nayo yako mbioni kupatikana.
Jacob aliongeza kuwa kukamilika kwa mchakato huo kutaongeza ufanisi katika uwajibikaji wa kuwatumikia wananchi kwani Manispaa ya Kindondoni imekuwa ikitoa huduma kwa idadi kubwa sana ya wananchi ila hali watendaji wake ni wachache hivyo inawagharimu kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humprey Polepole akitoa salaamu zake baada ya kukaribishwa katika Baraza hilo alisema kuwa wakati wowote shughuli za kiutendaji katikaWilaya ya Ubungo zitakuwa zikitolewa katika Ofisi zake kwani mchakato umekwisha kamilika.
“ Nifuraha yangu kuwa leo nipo hapa na watumishi wenzangu wengine inawezekana tukawa Ofisi moja katika wilaya yangu ya Ubungo, kwani nimearifiwa kuwa kila kitu kimekamilika hadi mgawanyo wa watumishi” Alisema Polepole.
Aliongeza kuwa anayo imani kuwa kazi iliyombele yake ni kuwatumikia wananchi wa Ubungo kwa kuwaletea maendeleo hivyo ni vyema akapata ushirikianao kwa wadau wote bila kujali itikadi zao.

Kuna namna mbili zipo zinazitwa “Political Power “ na zile “Political Development”; nisema tu mimi binafsi napenda tufanye Siasa ya Maendeleo kwa mustakabali wa Ubungo yetu. Alisema.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.