HII SI YA KUKOSA-TAMASHA KUBWA LA PAMOJA CARNIVAL KUFANYIKA DAR ES SALAAM LEADERS TAREHE 24 SEPTEMBER MWAKA HUU.

Ummy Majura ambaye ni mwakilishi kutoka Pamoja APP ambao ni wadhamini wa Tamasha kubwa la PAMOJA CARNIVAL litakalofanyika Tarehe 24 mwezi wa Tisa Jijini Dar es salaam akizngumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya Tamasha Hilo 
 Kampuni ya PURPLE COW MEDIA LTD ya nchini Tanzania leo imeta ngaza rasmi kuzindua kwa Tamasha kubwa Jijini Dar es salaam lililopewa Jina la PAMOJA CARNIVAL litakalofanyika katika viwanja vya Leaders Club kinondoni tamasha ambalo lina lengo la kuwaleta watu pamoja na kujifunza Njia Rahisi namna ya kijilinda na kuepuka ajali za Barabarani pamoja na kuburudika.
ANTONY KIZITO ambaye ni meneja masoko wa Quality Group ambao ni moja ya wafanikishaji wa Tamasha hilo akieleza mipango ya kufanikisha Tamasha Hilo.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es salaam Leo wakati wa kuzindua Tamasha hilo ANTONY KIZITO ambaye ni meneja masoko wa Quality Group ambao ni moja ya wafanikishaji wa Tamasha hilo amesema kuwa Tamasha hilo litafanyika tarehe 24 mwezi wa tisa mwaka 2016 ambapo watanzania watapata nafasi ya burudani na michezo mbalimbali,kushiriki kwenye maonyesho ya vipaji,ubunifu pamoja na biashara mbalimbali za wajasiriamali makampuni mbalimbali huku pia wananchi wakipata nyama choma na vyakula mbalimbali vya kiasili vilivyoandaliwa na wasanii wakubwa nchini hii ikiwa ni njia ya kuwahimiza kuwa Tanzania yenye neema bila ajali za hovyo inawezekana.
Bei Ya Viingilio unaweza kutizama hapo
Kizito ameongeza kuwa sababu kubwa ya lengo lao ni kutokana na ukweli kuwa ajali za barabaranbi zimekuwa zikiongezeka kila kukicha nchini Tanzania na kila mtanzania amekuwa akiguswa na madhara ya ajali hizo ikiwemo kupoteza ndugu na jamaa au marafiki,kupata ulemavu na hata uharibifu mkubwa wa mali hivyo tamasha hilo linatumika kuwaleta watanzania pamoja na kujua mbinu mbalimbali za kujikinga na madhara hayo.

Maswala mengine ambayo watanzania watapata kujifunza ni pamoja na matatizo yanayotokea kwenye aina za usafiri mbalimbali yakiwemo kusahau mizigo kwenye usafiri,ajali za kizembe,na kuporwa wakati wakusafiri ambapo katika tamasha hilo kutakuwa na makampuni mbalimbali ambayo yatatoa njia Mbadala wa kukabiliana na matatizo hayo.
 Kamishna msaidizi wa kikosi cha usalama Bara barabi nchini Tanzania FORTUNATUS MUSLIM ambaye alikuwa mgeni Rasmi akizindua Rasmi na kutia Baraka kufanyika kwa Tamasha hilo
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha hilo  Kamishna msaidizi wa kikosi cha usalama Bara barabi nchini Tanzania FORTUNATUS MUSLIM ambaye alikuwa mgeni Rasmi amepongeza Jitihada za kuanzishwa kwa mpango huo ambapo amesema utawasaidia wao kama wahusika katika jitihada zao za kupambana na ajali za barabarani nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa Kikosi cha usalama Barabarabi nchini Tanzania kimekuwa kikifanya Jitihada mbalimbali za kupambana na ajali za Barabarani hasa kwa Bodaboda ambapo sasa wameanzisha mashindano ya Mpira wa miguu maarufu kama Mpinga Cup ambayo yanalenga kuwakutanisha madereva wa Bodaboda wote Jijini Dar es salaam ili kujifunza njia za kuepukana na ajali ambapo amesema Tamasha la Pamoja Carnival limetia chachu katika Jitihada hizo.


Tamasha la Pamoja Carnival limedhaminiwa na FASTA FASTA ambao ni mfumo mpya wa usafiri Dar es salaam ambao utawahakikishia wasafiri uhakika wa usalama wa safari zao,uhakika wa mali zao,uhakika wa muda wao na madereva waaminifu.
Wadhamini wengine wa Tamasha hilo ni PAMOJA APP ambayo ni njia ya kisasa ya kuwakutanisha watu na wanaongea lugha ya Kiswahili nchini na Duniani kote pamoja na kutumia simu zao za mikononi ambapo APP hiyo inasaidia kuwakutanisha watu waliopotezana na kuongea na kubadilishana picha.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.