Friday, August 5, 2016

Mtanzania GELINE FUKO aliyesifiwa na OBAMA juzi kutoka LHRC awasili nchini Usiku wa leo,apata mapokezi makubwa kutoka wa wafanyakazi wenzake


Wafanyakzi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu LHRC wakiwa nanapkea kwa shangwe mfanyakazi mwenzao GELINE FUKO ambaye alikuwa nchini marekani kwa kushiriki Warsha ndogo iliyoandaliwa na Rais wa nchi Hiyo BARACK OBAMA ambapo katika shughulio hiyo mwanadada huyo alitajwa na Obama kama mtu ambaye amemvutia na mawazoi yake aliyoyafanya likiwa ni wazo lake la kuanzishwqa kwa Kanzi Data ya katiba nchini Tanzania wazo ambalo lilifanyiwa kazi na LHRC na kuwapa nafasi watanzania kusoma katiba kwa njia Rahisi zaidi.(Picha na Msaka Hbari Exaud Mtei)

Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Nchini Lhrc GELINE FUKO ambaye alipata Bahati ya kuwakilisha watanzania katika warsha maalum iliyoandaliwa na Rais wa marekani Barack Obama iliyokuwa na lengo la kuwakutanisha watu mbalimbali wakiwemo wanaharakati duniani wenye mawazo makubwa na mazuri  ambapo kwa Tanzania GELINE FUKO ndiye aliyewakilisha amerejea nchini usiku wa kuamkia leo na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa kutio hicho na watanzania wengine.
Geline Fuko ndiye aliyewasilisha wazo la kuanzishwa kwa Kanzi Data Maalum ndani ya Kituo cha LHRC ambayo ni maalum kwa ajili ya katiba ya Tanzania ambayo inawapa nafasi watanzania wote kupitia na kusoma katiba yao kupitia Data Base hiyo maalum na pia habari mbalimbali kuhusu mchakato wa katiba nchini  wazo ambalo limempa nafasi ya kushiriki katika warsha hiyo nchini marekani na kumfanya kujiletea sifa lukuki kwake na kwa Taifa kwa ujumla.

Katika shughuli hiyo moja kati ya mambo ambayo yaliwawavutia watu wengi ni pamoja na Rais Obama kumtaja Mtanzania huyo kama moja ya wanaharakati ambao amevutiwa na wazo lake la kuanzisha Kanzi Data ya katiba  na kumpa nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali na kujifunza Zaidi nchini Humo.


Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa Mwalimu Nyerere Dar es salaam GELINE amesema kuwa Wazo lake la kunzishwa kwa kanzi data ambayo imekuwa ina maswala yote kuhusu katiba na kuwapa watanzania wanafasi ya kusoma katiba yao kwa njia rahisi Zaidi wazo ilo lilitajwa na Rais Obama kuwa ni wazo bora na kuwazidi wengine waliokuwa wanatoka nchin mbalimbali.
Amesema kuwa Baada ya Obama kumtaja alipewa nafasi mbalimbali za kipekee ikiwemo yafasi ya kusoma katika vyuo vikuu viwili nchini marekani na kufundishwa na Maprofesa wakubwa nchini Marekani,nafasi ya kukuaa na Marais kadhaa wastaafu wa nchini Marekani na kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwao ambapo amesema ni bahati kubwa sana kwa mwanamke wa kitanzania kama huyo kuipata.

Naemi Silayo ambaye ni Mfanyakazi wa LHRC akizngunza katika mapokezi hayo amesema kuwa nafasi ya kwenda kushiriki katika warsha hiyo ilikuwa ni ngumu kupatikana kutokana na wingi wa watu waliokuwa wanaomba Africa na duniani kote lakini kutokana na ubora wa Wazo la GELINE alipata nafasi hiyo Adimu ya kuwakilisha watanzania wengine wote.

Wakizungumza katika mapokezi hayo baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa kituo hicho cha LHRC akiwemo mwanasheria PATIANCE MLOWE na Mkurugenzi wa fesha na utawala EZEKIEL MASANJA pamoja na kumpongeza kwa wingi sana Mfanyakazi mwenzao pia wamesema kuwa jambo hilo ni ishara ya kuwarudisha watanzania katika mjadala wa katiba mpya ambao umesahaulika kwa kipindi kirefu sasa na kuanza upya upatikanaji wa katiba kwa nchi ya Tanzania




No comments: