Saturday, August 20, 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ziara ya kukagua vituo vya Afya Wilaya ya Bunda

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Zahanati na vituo vya Afya katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara ambapo ametoa maagizo mbalimbali yafanyiwe kazi huku suala la watumishi likibainika kuwa ni tatizo katika Wilaya hiyo.

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea Zahanati ya Hunyari iliyopo Kijiji cha Hunyari, Zahanati ya Kihumbu, Maliwanda, Kituo cha Afya Mugeta, Zahanati ya Sanzate, Kituo cha Afya Ikizu.

Aidha, amewataka watendaji na Halimshahuri hiyo kuhakikisha wanakamilisha maboresho na utekelezaji mwingine ikiwemo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya kupanga safu ya ufanyaji wa kazi kwa kuwapeleka watalaamu katika Zahanati hizo ili kuwahudumia wananchi walio pembezoni.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Mh. Boniface alipongeza ziara hiyo kwani wameweza kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili sehemu ya utoaji wa huduma za Afya hivyo ujio wake huo kwenye maeneo hayo ya Vijijini yamewafungua macho.
DSC_6422
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitembelea kukagua shughuli za ufanyaji kazi wa Zahanati ya Hunyari
DSC_6429
Jengo maalum la wodi ya Wazazi la Zahanati ya Hunyari ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi

DSC_6440
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo kutoka Mkurugenzi wa Wilaya ya Bunda namna watakavyoisaidia Zahanati hiyo
DSC_6456
Mbunge wa jimbo la Bunda Vijijini, Mh.Boniface Mwita Getere akimtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi.Lydia Simeon Bupilipili
DSC_6461
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo na kupongeza wananchi wa kuweza kuchangia juhudi za ujenzi wa jengo la wodi la akinamama, Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi.Lydia Simeon Bupilipili
DSC_6471
moja la jengo la Zahanati ya Kihumbu ambalo nalo mejengwa kwa nguvu ya wananchi kama linavyoonekana ambalo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliweza kulitembelea kukagua ujenzi wake
DSC_6490 DSC_6520 DSC_6522 DSC_6527
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk. Jonathan Ezekiel Budenu ( Wa tatu kulia) afanyie haraka marekebisho ya upungufu wa wafanyakazi hasa maeneo ya vijijini
DSC_6541 DSC_6562
Mbunge wa jimbo la Bunda Vijijini, Mh.Boniface Mwita Getere akielezea jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Mugeta wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kituo hicho cha Mugeta
DSC_6586
moja ya jengo la Zahanati ya Sanzate ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi kama linavyoonekana pichani
DSC_6592
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua jengo hilo la Sanzate ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi
DSC_6596
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa watendaji wa kijiji cha Sanzate
DSC_6604 DSC_6625 DSC_6607 DSC_6655
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili kijiji cha Makongoro kukagua Kituo cha Afya Ikizu.
DSC_6664
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaonyesha bomba linalotakiwa kuwekwa katika chumba cha upasuaji wakati wa kuingia kwenye chumba cha upasuaji.
DSC_6672
msafara ukiendelea
DSC_6676
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo namna mashine kubwa ya kisasa ya ufuaji nguo ambayo ilitolewa na Wizara ya Afya ambayo hata hivyo Kituo hicho wameshindwa kuifanyia kazi.
DSC_6681
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa moja ya majokofu ya kuhifadhia mahiti kwenye kituo cha Afya Ikizu
DSC_6684 DSC_6701
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi Wheel chair kwa ajili ya wagonjwa wa kituo cha Afya cha Ikizu ambapo Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Boniface Getere alizitoa kama mchango wake
DSC_6704
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi Wheel chair kwa ajili ya wagonjwa wa kituo cha Afya cha Ikizu ambapo Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Boniface Getere alizitoa kama mchango wake
DSC_6712 DSC_6730ukaguzi ukiendeleaDSC_6742
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiaga wakati alipotembelea kwa karakana ya uchongaji ambayo ina historia ndefu..
DSC_6745
eneo la karakana ambayo ina historia ndefu ambapo jengo hilo ndipo palipochongwa kifimb cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
DSC_6748
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na viongozi wa Wilaya hiyo ya Bunda wakati wa kumaliza ziara hiyo ya kutembelea vituo vya Afya katika Wilaya ya Bunda.
 

No comments: