Sunday, August 14, 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla amezitaka taasisi za Dini kuubiri amani kwa jamii, kuombea Taifa

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaomba viongozi wa taasisi za Dini na viongozi wa dini hapa Nchini kuhakikisha wanaendeleza maombi kwa kuliombea Taifa suala la Amani ili Nchi kubaki katika misingi yake mikuu ya kuwaletea wananchi wake Maendeleo pamoja na kudumisha amani iliyopo.

Naibu Waziri Dk. Kigwangalla ameyasema hayo leo Agosti 14.2016 wakati alipokuwa mgeni rasmi kwa kumuakilisha Waziri wa Wizara hiyo. Mh. Ummy Mwalimu katika kufunga kongamano la Kimataifa la siku nne la SHILOH 2016, lililoandaliwa na Kanisa la Victorious Church Of Tanzania (VCT) lenye makao Makuu yake, Tabata Bima Jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo, Naibu Waziri aliweza kufunga rasmi kongamano hilo sambamba na kutoa sadaka kwa akina Mama Wajane sadaka zilizoandaliwa na kanisa hilo ilikuwasaidia akinamama Wajane mbalimbali.

Akitoa neno la kupongeza kwa uongozi wa kanisa hilo, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa, hatua ya kanisa hilo kuwajali Wanamama Wajane ni la kuungwa mkono kwani ni miongoni mwa mambo yanayopaswa kuigwa na watu wote ambapo pia kwa hatua yao ya kuliombea amani Taifa pamoja na viongozi wake ndilo jambo jema katika Nchi.
“Tunafanya kazi hii ya uongozi ni kwa uwepo wake Mungu kwani uongozi wetu sie ni Mungu ndiye aliyetaka tutumike na ndiye aliyetuita. Hivyo kufika kwangu hapa ni kuitika wito wa kuwatumikia watu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa neno kwa waumini huku akinukuu moja ya vifungu vya kwenye Biblia.

Ambapo pia amewataka viongozi hao kuendelea kuzidisha maombi kwa kuimbea Serikali ya Tanzania kwani kwa kipindi hiki ili Taifa liwe na amani pamoja na wananchi wake wafanye mambo ya kimaendeleo.

Aidha, katika hatua hiyo Dk. Kigwangalla alipata kuwafariji Wanawake Wajane ikiwemo kukabidhi baadhi ya zawadi kwa akina mama hao mchango uliotoka kanisani hapo.
Kwa upande wake, Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Bishop Elis Musa Chessa amemwelezea Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla kuwa ni miongoni mwa Mawaziri wenye upeo mkubwa hivyo katika dhama za sasa ni kati ya viongozi wanaohitajika katika kuinua Taifa kwani vigezo alivyo navyo vinatosha kabisa kwa kipindi hiki na kuendelea kwa miaka ya baadae.

“Tunaiombea Serikali yetu ya Tanzania kuwa na amani pamoja na viongozi wetu akiwemo Rais Dk. John Pombe Magufuli. Viongozi wote wa Serikali pamoja na Jamii nzima ya Tanzania” aliomba Bishop Elias Chessa.
Kongamano hilo la Kimataifa la Shiloh 2016, lilianza Agosti 11 na kufikia tamati siku ya leo Agosti 14 huku likikusanya waumini mbalimbali kutoka ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania.

Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokelewa wakati wa kuwasilia kwenye kanisa hilo la Victorious Church of Tanzania kufunga kongamano la siku nne la Kimataifa la Shiloh 2016, mapema leo Agosti 14.2016
DSC_5487
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea maua ya ukaribisho
DSC_5495
Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa akimtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akiwasili kanisani hapo kwa viongozi wa dini na wageni waalikwa

DSC_5499 DSC_5502

DSC_5504

DSC_5511

DSC_5525
Baadhi ya waumini wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kuingia ukumbini
DSC_5526
Baadhi ya waumini wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kuingia ukumbini
DSC_5528
Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa akitoa neno la shukrani katika tukio hilo
DSC_5530
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla katika kongamano hilo.
DSC_5536
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga rasmi kongamao hilo la Shiloh 2016
DSC_5540
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani
DSC_5565
Zoezi la kuwafariji Wamama Wajane likiendelea
DSC_5568
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwafariji baadhi ya Wanamama Wajane
DSC_5580
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwafariji baadhi ya Wanamama Wajane

No comments: