Samahani kwa baadhi ya Picha--Tizama Mauaji ya Polisi huko Mbagala ,Waziri Nchemba afika kushughudia
MAJAMBAZI WAMEVAMIA BENKI YA CRDB MAENEO YA MBANDE MBELE YA CHAMAZI NA KUUA MAASKARI 3 MUDA MFUPI ULIOPITA.......

WALIOFARIKI
E5761 CPL YAHAYA                                 F4660 CPL HATIBU NA
G9544 PC TTITO
KATIKA TUKIO LA UVAMIZI WA BANK MBANDE CRDB USIKU HUU SAA 19:3 0HRS. Inasemekana SMG moja wameondoka nayo majambazi. Tukio limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva. Majambazi hayakuingia ndani ya bank. Gari Leyland Ashok limeharibiwa sana kwa risasi. Ni tukio baya sana

 "Usiku huu nimefika Mbande-Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka  kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.


Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.


Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu."

Mwigulu Nchemba

23.08.2016

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.