Tuesday, August 23, 2016

TAZARA WAANDAA MAONYESHO MAALUM YA MIAKA 40 TANGU KUANZA SHUGHULI ZAKE


Katika kuadhimisha miaka 40 Tangu kuanza kutoa Huduma kwa mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA,wameandaaa maonyesho maalum yatakayofanyika katika makao makuu ya mamlaka Hiyo Jijini Dar es salaam kuanzia Tarehe 24-26 ya mwezi huu yakiwa na lengo la kuonyesha huduma na utendaji kazi wake kwa kipindi chote cha utoaji wa huduma yao.

Katika Taarifa iliyotolewa kwa wanahabari kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA Bwana Bruno Tandeo Chin’gandu  imeeleza kuwa katika maonyesho hayo watanzania watakaotemebea hapo watapata nafasi ya kujadili mijadala mbalimbali ikiwemo changamoto zinazokumba Sekta hiyo ya usafiri wa Reli nchini Tanzania ambapo wadau mbalimbali kutoka kila kona ya sekta hiyo watakuwepo kutoa Uzoefu wao juu ya maswala mbalimbali yakiwemo ya kisera,ya usafiri wa reli nchini.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa maadhimisho hayo ya miaka 40 yamekuja ikiwa si tu Tazara kueleza changamoto zake bali yamekuja kipindi ambacho Tazara imekuwa ikipigana kuhakikisha kuwa inasonga mbele kwa nguvu na kukabiliana na changamoto zote huku Taarifa hiyo ikiwakaribisha watanzania wote kutembelea maonyesho hayo yatakayoanza Tarehe 24 kujionea huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na mamlaka hiyo.

Maadhimisho ya miaka 40 yameanza takribani miezi miwili iliyopita  ambapo wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali kama Usafi katika maeneo mbalimbali katika Jamii na mahospitalini,kuchangia Damu kupitia mpango wa damu salama nchini,pamoja na kuwapokea wanafunzi na kuwaelekeza mambo mbalimabli juu ya Treni yao ya Abiria,

No comments: