Tuesday, August 30, 2016

TCRA CCC YAKABIDHI VYETI NA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUANDIKA INSHA NA MAKALA

Regan Yudos Kutoka shule ya msingi Mbuyuni akipokea cheti na zawadi ya mshindi wa Pili katika shindano la kuandika Insha kwa shule za msingi  aliyekabidhi zawadi hizo katika shughuli hiyo iliyofanyika katika Ofisi za Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano.leo tarehe 30 Agosti, 2016  ni Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu mawasiliano,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano Dr. Maria Sasabo  Kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa Baraza Bw. Satanley Mwabulambo, kushoto kwa Mwabulambo ni Mjumbe wa Baraza Bw. Lawrence Mworia na kulia kwa mgeni rasmi  Mary Shao Msuya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo.

Jane Michael Andrew mshindi wa kwanza katika shindano la kuandika Insha kwa shule za msingi akipokea cheti na zawadi kutoka kwa mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano Dr. Maria Sasabo leo Jijini Dar es salaam

Felician Crispin Kapama kutoka Zanaki Secondary mshindi wa pili shindano la kuandika Insha kwa shule za secondary akikabidhiwa zawadi zake leo wakati wa utoaji wa zawadi hizo uliofanyika Ofisi za Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Dar es salaam

Omary Abas Mdungu mshindi wa kwanza makala kwa vyuo vya elimu ya Juu akikabidhiwa zawadi zake Leo na mgeni Rasmi  Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano Dr. Maria Sasabo wakati wa Hafla hiyo fupi

Baraza la Ushauri kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania ( TCRA CCC) leo limekabidhi vyeti na zawadi kwa washindi walioshiriki katika shindano la uandishi wa insha kwa shule za msingi na sekondari na makala kwa vyuo vya elimu ya juu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Mashindano hayo yalihusisha washiriki kuandika insha na makala juu ya haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano hapa nchini.


Akikabidhi vyeti na zawadi hizo kwa washindi mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano DK. Maria Sasabo amesema amehamasika kuona vijana wameshiriki katika mashindano hayo na kutoa maoni juu ya faida, changamoto na mbinu mbali mbali za kukabiliana na changamoto hizo katika kuboresha utoaji wa huduma kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano.

Aidha, Dr. Sasabo ametoa rai kwa vijana kutumia fursa mbali mbali zitokanazo na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano kukuza vipaji, kujielimisha na pia kupata ajira.

Pia, amewaasa vijana kutumia huduma mbali mbali za mawasiliano kwa kufuata sheria na kanuni za nchi kwa ustawi wa wao kielimu, kijamii na kiuchumi.

No comments: