Tuesday, August 9, 2016

TIGO, KUPATANA.COM KUSHIRIKIANA KUWEZESHA BIASHARA KWA MTANDAO

 Meneja Miradi wa Tigo, Anthony Njau (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Dar es Salaam leo aasubuhi kuhusu kampuni hiyo na Kampuni ya ya Kupatana.com, kushirikiana kuwezesha biashara kwa mtandao. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kupatana.com, Philip Ebbersten na kushoto ni Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Makusaro Tesha. 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Kupatana.com, Philip Ebbersten (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Makusaro Tesha (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.


Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania na kampuni ya Kupatana.com, moja ya kampuni zinazoongoza Tanzania  katika huduma za masoko katika mtandao  zimeingia katika ubia wa kibiashara ambapo kila kampuni  itauza bidhaa na huduma za  kila mmoja katika majukwaa yao ya kidijitali.

Katika hatua za mwanzo za ushirikiano huu, Kampuni ya Tigo Tanzania itachagua maduka matatu ambayo Kupatana.Com itayatumia kuwawezesha wateja wa Tigo kuuza simu zao zilizotumika kwa kupitia jukwaa la Kupatana.com.

Akizungumza wakati wa  kusaini makubaliano baina ya pande hizo mbili jijini Dar es Salaam,  Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Tigo, Anthony Njau  alisema, “tukiwa ni kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali, tumeona kwamba hivi sasa Watanzania wamehamasika mno katika kufanya biashara kupitia njia ya mtandao.”Njau aliongeza kwamba , “Mtandao na wavuti wa Kupatana.com unatoa jukwaa zuri ambalo linabadilisha  namna ambavyo watu wanaishi kwa kuwezesha kupatikana kwa  huduma na bidhaa katika njia sahihi na rahisi.”

“Lengo la muda mrefu ni kuwapatia wateja wetu jukwaa  ambalo wanaweza kupakua  vifaa ambavyo vilishatumika ili kuviboresha na kwa upande wa Tigo kuuza  vifaa vipya, kuongeza usambazaji  na kuwa na mafanikio katika  jaribio hili la msingi, Tigo na Kupatana.com zitapanua wigo wa huduma hii na kuhakikisha inapatikana kwa urahisi katika maduka yote 52 ya Tigo  ambayo yamesambaa  kote nchini,” alisema Njau.

 Mkurugenzi wa Kupatana.com, Philip Ebbersten, alisema kwamba kupitia matumizi ya jukwaa hilo, wauzaji (kampuni na watu binafsi) wataweza  kuwafikia maelfu ya  wanunuzi muhimu kila siku bila kujali  maeneo yao ya kijiografia.

Alifafanua kuwa kuorodhesha bidhaa katika jukwaa hilo  ni bure  na kuwashauru wateja umuhimu wa  kufuata kanuni  na miongozo salama kwa bidhaa zote zitakazotangazwa Kupatana.com ili waweze kuzitapa  kwa usalama na uelewa zaidi.


No comments: