Sunday, August 14, 2016

UMESKIA MANENO MAPYA KUTOKA KWA KATIBU MKUU CHADEMA JUMAPILI HII KUHUSU UKUTA,SOMA HAPA



Na Mashinji VB ( Katibu wa CDM)
Nimejaribu kufuatilia sana mwenendo wa safari ya Rais JPM...kwa kweli kajichanganya sana na sijui anataka mimi nimweleweje!

Akiwa Mkoani Singida "Wanaotakiwa kufanya siasa ni wale waliopewa ridhaa na wananchi tu, na lazima wafanye siasa kwenye majimbo au kata zao tu. Yeye jimbo lake ni Tanzania nzima. Atafanya siasa nchi nzima"
Sijui kama rais anaikumbuka sheria namba 5 ya 1992 inayohusu vyama vya siasa.


Akiwa Mkoani Mwanza katika mkutano wa hadhara pale Furahisha, rais alitoa nafasi kwa wabunge wasio wa Ilemela kuhutubia. Alienda mbali zaidi na kumpa nafasi Katibu Mkuu wa ADA-TADEA kusalimia na kuhutubia wananchi.

Wabunge wamefanya siasa nje ya maeneo yao. Rais kashindwa kusimamia kauli yake aliyotoa Singida ndani ya wiki moja!
Kwa nini unaweka marufuku ambayo hata wewe inakushinda kutekeleza?

Sasa naona kwa nini ni muhimu kujenga UKUTA.
UKUTA ni nini?

UKUTA ni operasheni inayokufanya wewe Mtanzania kubadili mtazamo wako katika mwenendo wa uongozi wa nchi yetu. Kama Mtanzania, unatakiwa ujihoji na uhoji kwa nini hiki, na kwa nini kile?

Usikae tu na kusubiri kwamba kuna watu wa maana sana watafikiri na kufanya maamuzi kwa niaba yako. UKUTA ni dhana inayokufanya wewe kama mwananchi ufuatilie kila jambo linalotendeka ndani ya Taifa na kutoa maoni yako kwa uhuru kabisa bila kuingiliwa.


UKUTA ni fikra, na fikra huwezi kuizuia. Kwa namna gani watu watatambua unawaza nini? Ni kwa kukutana na kuongea. Ndiyo maana sheria namba 5 ya 1992 pamoja na kanuni zake inatoa uhuru na haki ya kukutana na kuandamana. Ukibadili fikra yako na kuona ukweli huu, basi utajiunga nami katika kujenga UKUTA imara. Usigubikwe na gilba za "HAPA KAZI TU, FIKIRA MARUFUKU" kwani hakuna kazi unayoweza kuifanya bila mipango; na mipango inatokana na fikira pana.

UKUTA unajengwa.

No comments: