Sunday, August 21, 2016

USIKU WA LEO--Kasesela awasweka ndani walinzi 2 wa kampuni ya Amazon security kwa kunyanyasa wananchi


 Leo saa 3 na dakika 25 Usiku mkuu wa wilaya Mh Richard Kasesela alipokea wakina mama 3 wakiwa wanatetemeka kwa baridi, wakilalamika kumwagiwa maji walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa walio lazwa hasa kwa wale walio toka mbali. Maji hayo yalimwagwa na walinzi wa kampuni ya Amazon ambao ndio wamepewa kandarasi ya ulinzi hospitali ya Rufaa ya Iringa..

Mkuu wa wilaya alifika hospitali kujionea mwenyewe hali halisi, baadae pia akapata taarifa kuwa jana yake Mlinzi alimpiga mzee aliyekuwa ameleta chakula hospitali na kumwaga kwa mateke. Mkuu wa wilaya aliamuru mlinzi huyo na mwenzake wakamatwe pia mwenye kampuni afike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo. "Hali hii imeudhi sana hasa ukiona jinsi wakina mama walivyo nyanyasika wengine vyombo vyao na chakula kuroweshwa maji." alisema Mh Kasesela.
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO







No comments: