Tuesday, September 27, 2016

HELA ZA TETEMEKO ZAONDOKA NA MKURUGENZI WA BUKOBA,MHASIBU PIA ATUMBULIWA

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha.

Aidha, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.
Hata hivyo Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya "Kamati Maafa Kagera" ambayo imetangazwa na Serikali.

No comments: