Thursday, September 22, 2016

Hii Ndiyo Agenda inayojadiliwa UN kuhusu Malalamiko ya Maalim Seif wa CUF huko Zanzibar


ZIARA ya kimataifa aliyoifanya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Marekani, Ulaya, Canada na Umoja wa Mataifa kulalamikia uvurugaji wa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba mwaka jana, imeanza kuzaa matunda,

Tayari taasisi ya kimataifa ya umoja wa wanaliberali – Liberal International (LI) – imeliandikia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) kutaka kutolewa kwa vikwazo dhidi ya Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye tovuti ya LI, taasisi hiyo imetaka baraza hilo lenye jukumu la kulinda misingi ya haki za binadamu kwenye mataifa yote wanachama wa UN, kuchukua hatua kali ili kukomesha “uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu na ukandamizaji wa haki za kisiasa na kiraia visiwani Zanzibar.”
ya kupinga walichokiita “uonevu wanaofanyiwa viongozi wa upinzani Zanzibar na wafuasi wao.”

“Tunaitaka serikali ya Zanzibar na Tanzania kuheshimu utawala wa sheria na kuingia katika majadiliano na upinzani ndani ya muda maalum hatua ambayo itawezesha kuundwa serikali ya mpito na kukubali kuitishwa kwa uchaguzi mpya ili kuondoa mgogoro uliojitokeza baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015,” imesema taarifa ya LI
 



No comments: