Wednesday, September 14, 2016

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania aumwagia sifa Mradi wa TYEEO Barazani na kuahidi kutoa ushirikiano.

fis1Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bibi. Joyce Fissoo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Kampuni ya Barazani Entertainment mara baada ya kikao cha kutambulisha  Mradi wa  TYEEO Barazani, leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo unalenga kuinua vipaji vya wasanii wa Filamu nchini, ambapo Mradi huo utasaidia klusambaza kazi za wasniii wa Filamu kwa njia ya kisasa.
Picha na Frank Shija, MAELEZO
fis2Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bibi. Joyce Fissoo akizungumza wakati wa kikoa baina yake na Ujumbe kutoka Kampuni ya Barazani Entertainment walipofika ofisini kwa ajili ya kutambulisha Mradi wa  TYEEO Barazani leo Jijini Dar es Salaam.Mradi huo unalenga kuinua vipaji vya wasanii wa Filamu nchini.
fis3Mkurugenzi Mtendaji wa Barazani Entertainment Bw. John Kallaghe (wapili kulia) akifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (hayupo pichani) wakati wa kikoa baina yake na Ujumbe kutoka Kampuni ya hiyo walipofika ofisini kwake  kwa ajili ya kutambulisha Mradi wa  TYEEO Barazani, leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo unalenga kuinua vipaji vya wasanii wa Filamu nchini kupitia usambazaji wa kazi zao kwa njia ya kisasa.
fis4Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bibi. Joyce Fissoo akifuatilia hoja kutoka kwa mmoja wa wajumbe kutoka Kampuni ya Barazani Entertainment walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kutambulisha Mradi wa TYEEO Barazani, leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo unalenga kuinua vipaji vya wasanii wa Filamu nchini kupitia usambazaji wa kazi zao kwa njia ya kisasa, Kushoto ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Abuu Kimario.
fis5Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bibi. Joyce Fissoo akiwa ameshika Fulana yenye utambulisho wa Mradi wa TYEEO Barazani wakati wa kikoa baina yake na Ujumbe kutoka Kampuni ya Barazani Entertainment walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kutambulisha Mradi wa  huo, leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo unalenga kuinua vipaji vya wasanii wa Filamu nchini kupitia usambazaji wa kazi zao kwa njia ya kisasa. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza Entertainment Bw. John Kallaghe.

No comments: