MBEYA CITY IMERUDI MAHALA PAKE,YAIADHIBU MBAO FC GOLI 4-1IMG- Copy 11Licha ya kucheza kwenye uwanja wa  nyumbani, Mbao  Fc ya Mwanza  imejikuta  ikishindwa  kuhimili  vishindo vya Mbeya City Fc na kukubali kufungwa  mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania  bara  uliochezwa  leo hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba  jijini hapa.
Kwenye Mchezo huo  ulioanza kwa kasi  timu zote zikishambuliana kwa zamu, wenyeji walikuwa wa kwanza kulifikia lango la City  baada ya Vicent Philipo kufanikiwa kumtoka Haruna Shamte aliyekuwa anacheza beki ya kulia  lakini mpira wa krosi wa mchezaji huyo wa Mbao  uliishia  mikononi mwa kipa Owen Chaima.
City ilijibu shambulizi kwenye dakika ya 20 kupitia Ayoub Semtawa  aliyefanikiwa  kuwatoka walinzi wa Mbao Fc lakini mpira aliompenyezea Omary Ramadhani uliokolewa na walinzi wa timu hiyo mwenyeji kabla  ya  Raphael Daud  kufanikiwa kuandika bao la kwanza  baada ya kuunganisha  mpira  ulikuwa umepigwa na Ayoub Semtawa kwenye dakika ya 28, bao lililodumu kwa dakika 10  baada ya Vicent Philipo kuswazisha  dakika ya  38 na kumaliza kipindi cha kwanza timu zote zikiwa na bao 1-1.
Kipindi cha pili Kocha Kinnah Phiri alifanya mabadiliko  ya kumtoa alifanya mabadiliko ya kumtoa  Ayoub Semtawa na nafasi yake kuchukuliwa na Ditram Nchimbi  mabadiliko ambayo  yaliongeza  uhai kweny safu ya ushambuliaji kwani  dakika chache baadae Omary  Ramadhani aliiandika  bao la pili, bao lilofuataiwa na mabao mengine mawili kutoka kwa Ramadhani Chombo na Raphael Daud waliohitimisha dakika 90  ubao ukisomeka  mabao 4 kwa City na 1 kwa Mbao Fc.
Mara baada ya mchezo huo kocha wa City  Kinnah Phiri, pamoja na mengine mengi lakini pia  aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizui kwa kufuata Maelekezo na hatimaye  kuibuka na ushindi  huo mnono.
“Vijana wangu wamecheza  vizuri,  wamefanya kazi kwenye kila tulichokuwa tunakifanyia mazoezi, tulijua Mbao wangekuja na mchezo wa kasi kwa sababu walihitaji sana  kushinda hasa baada ya kupoteza mchezo wao uliopita,  tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha  kupata pointi saba kwenye michezo yetu mitatu na sasa tunarudi nyumbani kujiandaa na mchzo mwingine”, alisema.
Dondoo za mchezo,mahojiano ya Kinnah Phiri yapo hapa : http://mbeyacityfc.com/event/mbao-fc-vs-mbeya-city/
City  itaondoka Mwanza  alfajiri ya kesho kuelekea jijini Mbeya tayari kwa matayarisho ya mchezo dhidi ya Azam Fc  uliopangwa  kuchezwa  tarehe 10 mwezi huu kwenye uwanja wa Sokoine.
IMG-20160903-WA0027Haruna Shamte(katikati) Rajab Zahir (kushoto) wakishangilia bao la pili lililofungwa na Omary Ramadhani (Kulia)

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.