Thursday, September 29, 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ziara Wilaya za Buhigwe na Uvinza Mkoani Kigoma


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya za Uvinza na ile ya Buhigwe na kutembelea Hospitali na vituo vya Afya ndani ya Mkoa huo wa Kigoma.
Akiwa katika kituo cha Afya cha Uvinza,  Naibu Waziri  ameweza kubaini mapungufu mbalimbali huku na kutoa maagizo kwa wasimamizi wake kuhakikisha wanafanyia marekebisho kasoro hizo kwa muda unaotakiwa kabla ya kuchukuliwa  wahusika.
Miongoni mwa kasoro  alizobaini ni pamoja na kuwa kituo hicho licha ya kuhudumia wananchi kama Hospitali ya Wilaya ya Uvinza, hadi sasa  hakina sifa hiyo kwani  hakina Chumba cha upasuaji, Maabara hisiyofuata utaratibu pia kutokuwa na maji kwa kituo hicho maji ambayo wanategemea kutoka kwa wagonjwa.

“Kituo cha Afya Uvinza, kinahudumia eneo lenye watu zaidi ya 59,000. Walipaswa kuwa 10,000 tu. Hakina maji, umeme Kwa sababu zisizo za kawaida. Hakuna Chumba cha upasuaji (Theatre), maabara ya kusuasua na dawa si za kutosha.
 Nimewaagiza ndani ya miezi mitatu wawe wamekarabati eneo nusu la wodi ya wanaume kiasi cha kuweka  Chumba cha Upasuaji.  Pia wavute maji na kuweka matenki juu ili kuepukana na tabia ya kuagiza wajawazito kuja na ndoo za maji kituoni!.  Nimewapa mwezi mmoja ili wavute umeme na kuanza kutumia Vifaa vyao Vya maabara.” Amesema Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo yake hayo kwa viongozi wa Serikali na wa Hospitali hiyo.
Aidha, kwa upande wa ziara yake katika Wilaya ya Buhigwe, Dk. Kigwangalla alipongeza juhudi za wabia binafsi kwa kuweza kushirikiana na Serikali kwenye jambo la maendeleo huku akiwahakikishia uongozi wa Hospital ya Wasabato ya Heri Mission  iliyopo eneo la Manyovu  kuwa juhudi zao wanazitambua na suala la kuifanya Hospitali hiyo kuwa Hospitali teule ya Wilaaya zinashughulikuwa huku akiwataka kuzingatia sheria mbalimbali na mambo madogomadogo.
Dk. Kigwangalla ameutaka uongozi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanafanyia marekebisho ya barabara inayoingia Hospitalini humo pamoja na kuhakikisha wanajenga vituo zaidi vya  Afya ili kuwafikia wananchi wake.
Dk. Kigwangalla yupo Mkoani hapa  kwa ziara ya siku ambapo pia atatembelea Hospitali na vituo vya  Afya vya Kigoma Mjini.
mwisho.

No comments: