TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU UZINDUZI WA MAJENGO YA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO


indexjeshi la polisi mkoa wa mbeya linapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa kutakuwa na uzinduzi wa majengo ya ofisi za dawati la jinsia na watoto zilizopo polisi kati mbeya na kituo kidogo cha polisi ilomba.uzinduzi huu utafanyika tarehe 30.09.2016 siku ya ijumaa.

majengo hayo ya ofisi za dawati la jinsia na watoto ni moja kati ya majengo yanayojengwa nchi nzima katika kutekeleza mpango mkakati wa kujenga miundo mbinu ya ofisi za dawati la jinsia na watoto unaofadhiliowa na unicef.
hivyo wananchi mjitokeze kwa wingi katika kushuhudia tukio hilo muhimu na la kihistoria katika mkoa wetu wa mbeya.
mgeni rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa mbeya mh. amos makala
kauli mbiu:- funguka tumia dawati la jinsia na watoto kutokomeza ukatili wa kijinsia.
imetolewa na.

ofisi ya kamanda wa polisi
mkoa wa mbeya.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.