Washiriki wa kinyang’anyiro cha
kumsaka mrembo wa elimu ya juu kwa mwaka 20016 (TTCL Miss Higher Learning 2016)
kwa kushrikiana na jeshi la pilisi kitengo cha usalama barabarani wametoa elimu
ya matumuzi sahihi ya alama za barabarani pamoja na kuwavusha barabara baadhi
ya wanafunzi toka katika baadhi ya shule zilizopo katika jiji la Dar es Salaam
ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika kwa shindano hilo.
Miongoni mwa shule ambazo
zimepata fursa ya kutembelewa na washiriki wa TTCL Miss higher learing ni Shule
ya Msingi Mbuyuni, Shule ya msingi Osterbay, Shule ya Msingi Uhuru
Mchanganyiko, Shule ya Msingi Mtoni, na Shue ya Msingi Mgulani.
Akizungumza na wanahabari muandaaji
shindano la TTCL Miss higher learing, Maya Kitambo amesema lengo hasa la
kufanya zoezi la kuwavusha barabara pamoja na maswali ya ufahamu juu ya sheria
na alama za usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha
usalama barabarani ni ili kutoa msisitizo kwa wanafunzi wa shule za msingi
kuzifahamu alama na sheria ili kuepusha ajali ambazo huwahusisha wanafunzi
wawapo barabarani.
“Sisi kama AJ Events tumeguswa
katika utoaji wa elimu kwa wanafunzi pamoja na kuwavusha barabara kwani
tunaamini kwamba kupitia washiriki wetu TTCL Miss higher learing, wanafunzi
wataona umuhimu wa kuzijua sheria pamoja na kuwa makini wawapo barabarani”
amesema Maya Kitambo.
Washiriki watakaoshiriki katika
shindano hilo litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon Hall uliopo Namnaga
ni Glory Gideon (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Lucy Ludy (TAASISI YA USTAWI
WA JAMII), Jonatha Joram (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Clara Nyaki
(TAASISI YA USTAWI WA JAMII), Rhoda Iddy (CBE), Evelyne Andrew (TAASISI YA
USTAWI WA JAMII), Tamita Mwakitalu (CHUO CHA UTUMISHI WA UMA MAGOGONI),
Jackline Everist (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Nasra Muna (Chuo cha
Usimamizi wa fedha IFM) Laura Kwai (Iringa University), Mariam J Mwita (CHUO
CHA UTUMISHI WA UMA MAGOGONI), Emmaculate Kasinsa (CHUO CHA UTUMISHI WA UMA
MAGOGONI), Victoria Shiyo (CBE), Farida mlawa (UDOM), Lilian Kaishozi (UDOM).
Wakati huohuo Msanii wa muziki wa
kizazi kipya Hellen George Rubb pamoja na Navy Kenzo watatoa burudani katika
shindano hilo kwa kiingilio katika shindano hili ni shilingi 50,000 kwa VIP
pamoja na shilingi 10,000 kwa viti vya kawaida.
No comments:
Post a Comment