Monday, October 31, 2016

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe 31 Oktoba 2016.

http://tanzaniainvest.com/wp-content/uploads/2015/12/dse-dar-es-salaam-stock-exchange-tanzania.jpg
                       Mauzo ya Soko
Idadi ya mauzo imeongezeka kwa asilimia 39% na kufikia TZS 5.3 Bilioni kutoka TZS 3.8 Bilioni wiki iliyopita.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeshuka kwa asilimia 91% hadi 869,453 kutoka 9.8 Milioni wiki iliyopita.
Kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     CRDB kwa asilimia 51.8%
2.     TBL kwa asilimia 44.44%
3.     DCB kwa asilimia 1.22%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa asilimia 1% na kufika Trilioni 21.8 kutoka Trilioni 21.6 wiki iliyopita.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia umepanda kwa asilimia 0.4% hadi Trilioni 8.19 kutoka Trilioni 8.16 wiki iliyopita.

Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda imejitokeza wiki hii kuongezeka Zaidi ya pointi 26 baada ya bei ya hisa za TBL kuongezeka kwa asilimia 0.76%:

Bei za hisa za makampuni mengine ya ndani ziliendelea kubaki kwenye kiwango kile kile na kupelekea viashiria vya sekta za huduma za kibenki na za kibiashara kubakia kwenye kiwango kile kile wiki hadi wiki.
. by Exaud Msaka Habari on Scribd

No comments: