Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Issa Hayatou ameteua
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa
miongoni mwa wajumbe 11 wa Kamati maalumu ya mageuzi ya muundo wa CAF
itakayokuwa na jukumu la kufanya mabadiliko mapya ya shirikisho,
imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, katika Kamati hiyo ikayoongozwa na Rais
Issa Hayatou mwenyewe, Malinzi ameteuliwa katika Kamati hiyo
iliyotangazwa leo Oktoba 30, 2016 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Kamati hiyo imeundwa ikiwa ni sehemu ya maazimio ya mkutano uliopita
wa kawaida wa CAF uliofanyika Septemba 29, mwaka huu ambako Rais Hayatou
amezingatia mjadala uliolenga kufanya mabadiliko CAF kwa kufanyia kazi
mara moja.
Hayatou si tu kwamba amejali mjadala wa mkutano ule, pia ameheshimu
mawazo ya vyama wanachama vya nchi pamoja na wajumbe wa Kamati ya
Utendaji na wataalamu mbalimbali ili kupata mustakabali wa muundo wa
uongozi wa shirikisho hilo ili kukabiliana na changamoto dhidi ya mpira
wa miguu barani Afrika.
Akizungumzia uteuzi huo, Malinzi kwanza alimshukuru Hayatou kwa
uteuzi huo ambao umeonyesha moja kwa moja kuwa na imani naye katika
kuleta maendeleo ya mpira wa miguu katika muundo mpya.
“Lakini sifa hii ya kuteuliwa ni yangu pekee kwani ni heshima kubwa
ambayo imepewa nchi yetu pendwa ya Tanzania, kadhalika nchi zote za
Afrika Mashariki na Kati,” alisema Malinzi alipozungumza namtandao wa
TFF ambao ni www.tff.or.tz.
Kamati hiyo itawajibika kwa Kamati ya Utendaji ya CAF ili kupata mwongozo ingawa haibanwi zaidi na Katiba ya shirikisho.
Kamati inaundwa na:
1. Issa Hayatou (Cameroon), ambaye ni Rais CAF atakayekuwa Mwenyekiti.
2. Amadou Diakite (Mali), Makamu Rais wa CAF na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho.
3. Mohammed
Raouraoua (Algeria), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji CAF ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Masuala ya Sheria. Pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu la Algeria (FAF).
4. Lydia Nsekera (Burundi) Mjumbe wa Baraza la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
5. Raymond Hack (Afrika Kusini), Mwenyekiti wa Bodi ya Nidhamu ya CAF.
6. Me. Prosper Abega (Cameroon), Mwenyekiti wa Bodi ya Rufaa ya CAF.
7. Jamal Malinzi (Tanzania), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
8. Me. Augustin Senghor (Senegal), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Senegal (FSF)
9. Victor Adolfo Osorio (Cap Verde), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Cap Verde (FCF)
10. Maclean Letshwti (Botswana), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Botswana (BFA)
11. Hicham El Amrani (Morocco) ambaye ni Katibu Mkuu wa CAF.
No comments:
Post a Comment