Oktoba Mosi (1) ya kila
mwaka ni siku iliyoteuliwa na Umoja wa Mataifa kuadhimisha uwepo wa wazee
katika jamii kote ulimwenguni. Siku hii ilianza kuadhimishwa rasmi Oktoba 1,
1991 kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu mambo yanayowalenga wazee ikiwemo
kutoheshimu haki za wazee, kutazama mahitaji na maslahi ya wazee na kuhakikisha
mzee popote alipo ulimwenguni anapata huduma za msingi za kijamii kama vile huduma
bora za afya na matibabu.
Mahususi, siku hii imekuwa
na lengo la kuutambua mchango wa wazee katika jamii kwa wakati husika na wakati
uliopita katika mataifa yao. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu tunatumia
fursa hii kuwapongeza wazee wote duniani na hususan wazee wa Tanzania.
Pia
tunatumia siku hii kuikumbusha serikali
na mihimili mingine ya dola pamoja na wanachi wote kwa ujumla kuheshimu wazee wetu kama hazina ya taifa.
Pia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaitumia siku hii kuungana pamoja na
wazee wanaodai haki yao kwa zaidi ya miaka 20.
Mathalani, wazee waliotumikia
iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuvunjika kwake mwaka, 1977
ambao mpaka leo wameendelea kupambana na kudai haki yao.
Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu pia tunaitumia siku ya leo kuitaka serikali ya Marekani kupitia
Ubalozi wake nchini Tanzania kutoa msimamo wake juu ya kesi ya madai ya
waliokuwa walinzi wa ubalozi wa marekani nchini Tanzania wakijulikana kama
'mission security force' katika Ubalozi wa Amerika kwa serikali ya Amerika –
1984.
Sambamba na hayo Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu kinakemea vikali vitendo vya mauji ya wazee kwa
imani za kishirikina vinavyozidi kupamba moto nchini, watoa huduma wa afya
wanaotumia lugha za kuudhi dhidi ya wazee, vijana wanaorubuni wazee kuuza mali
zao na kuwatapeli hususani ardhi kuacha vitendo hivi ili kuheshimu tunu hii
adhimu ya taifa..
Wazee ni hazina kwa Taifa
tuilinde hazina hii kwa uendelvu wa jamii yetu.Tuwatunze na kuwasikiliza wazee
wetu.
Imetolewa Leo Tarehe
1/10/2016
Dkt.Helen Kijo-Bisimba
Mkurugenzi Mtendaji
No comments:
Post a Comment