UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayofuraha kuwaataarifu wapenzi wa soka kuwa jioni ya leo umefanikiwa kuingia mikataba na wasshambuliaji nyota kutoka Ghana, Samuel Afful na Yahaya Mohammed.
Zoezi la kuingiana mikataba limehudhuria na baadhi ya viongozi wakuu wa timu wakiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, Meneja Mkuu, Abdul Mohamed, Kocha Mkuu Zeben Hernandez pamoja na wakala anayewasimamia wachezaji hao, Kingsley Atakorah, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Adom Wonders Academy ya nchini Ghana.
Wakati Afful, 20, akisaini mkataba wa miaka mitatu, Mohammed aliyetua nchini leo mchana akitokea Ghana naye amesaini kandarasi ya miaka miwili tayari kabisa kuanza kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Afful ambaye mpaka sasa yumo katika vikosi vya timu za vijana za Ghana chini ya umri wa miaka 20 na 23, anajiunga Azam FC akitokea timu ya Sekondi Hasaacan ya Ghana, ambayo aliifungia mabao tisa timu hiyo msimu uliopita.
Mohammed ambaye ni mshambuliaji mzoefu anayetokea Aduana Stars, alikuwa ni mfungaji bora namba mbili wa Ligi Kuu ya Ghana msimu uliopita akifunga mabao 15, pungufu ya mabao mawili na kinara Latif Blessing (Liberty Proffessional) aliyetupia 17.
Azam FC tunapenda kuwafahamisha mashabiki wetu kuwa tutaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi kwa kukifanyia marekebisho kikosi chetu katika usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa jana, lengo ni kukipa nguvu zaidi kikosi chetu bili kifanye vizuri zaidi katika michuano ya hapa nchini pamoja na ile ya Kimataifa.
Imetolewa na Uongozi wa Azam FC
No comments:
Post a Comment