Thursday, November 17, 2016

Benki ya AMANA yazindua Huduma ya Mikopo midogo midogo kwa wafanya Biashara Mbagala Jijini Dar es Salaam

Diwani wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es salaam Mh Abdala  Mtimika (Kushoto) Pamoja na Mkurugenzi wa Bank ya Amana nchini Dr Mosen Masoud wakikata utepe Kuashiria kuzinduliwa Rasmi kwa Huduma ya mikopo Midogo Midogo kwa wafanya biashara wa Mbagala Jijini Dar es salaam.uzinduzi huo umefanyika katika Tawi la Amana Mbagala(Picha zote na Vicent Macha wa Habari24 blog)
 Hatimaye wakazi wa mbagala wanaofanya Biashara ndogo ndogo wakiwemo wajasiriamali wamepata neema kubwa baada ya Bank ya AMANA kuzinduaa huduma yake mpya ya kutoa mikopo midogo midogo kwa wafanya biashara, huduma ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni miaka mitano Tangu kuanzishwa kwa Bank Hiyo.
Akizungumza na wanahabari na wananchi wa mbagala ambapo ndio uzinduzi huo umefanyika Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen Masoud amesema kuwa huduma hiyo imeanzishwa mahususi kwa kutambua hitajio kubwa katika jamii la wafanya biashara wadogo wadogo katika kupata mtaji ya kukuza biashara zao hivyo Bank ya Amana imeamua kuwainua wafanya biashara hao wadogo ili kuinuka kipato chao na kufikia kipato cha kati na hata kipato cha juu.


Amesema kuwa kupitia huduma hiyo Amana Bank inawawezesha wafanya biashara kwa kununua bidhaa wanazohitaji katika biashara zao na kuwauzia kwa bei nafuu kwa mkopo ambapo watarejesha kidogo kidogo katika muda ambao umewekwa katika utaratibu.
Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen Masoud akizungumza na wanahabari na wananchi waliofika katika uzinduzi huo 
Ameongeza kuwa wafanyabiashara sasa wana nafasi ya kukodishwa vifaa mbalimbali wanavyohitaji katika kuendesha biashara zao kwa kodi nafuu na mwishowe wanaweza wakanunua vifaa hivyo kwa Bei nafuu
Mkurugenzi huyo ameendelea kueleza kuwa kwa sasa Huduma hiyo ya mkopo imeanza kutolewa kwa wateja wake wanaotumia Tawi lao la Mbagala tu lakini kusudi lao ni kuhakikisha kuwa wanaendesha zoezi hiyo latika matawi yao yote nchini ambayo kwa sasa yapo matawi saba.
Diwani wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es salaam Mh Abdala  Mtimika Akizungumza 
Akizunguza wakati wa uzinduzi huo Mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa kata ya Kibondemaji Abdala Mtimika ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Temeke amesema kuwa Uzinduzi wa Huduma hiyo ya kutoa mikopo midogo modogo sasa imekuja wakati muafaka kipindi ambacho watanzania wengi wamekuwa wakilalamika kudorora kwa uchumi na pesa kupotea hivyo ni jukumu la wafanya biashara wa mbagala kutumia nafasi hiyo adhimi kuhakikisha kuwa wanapata mikopo hiyo na kuwekeza katika Biashara zao.
Wiki ya Huduma kwa wateja ikiendelea wateja mbalimbali wakipata Huduma katika Tawi la Benk hiyo Mbagala leo
Aidha Diwani huyo amewapongeza sana uongozi wa Bank ya Amana Tanzania kwa kuweza kuendesha Bank hiyo kwa usawa pamoja na kuwa imekuwa ikijulikana kuwa Ni Bank ya kiislam ila sio kweli kwani imekuwa ikitoa Huduma kwa watanzania wote bila kujali Dini zao pamoja na kuwa inatumia Taratibu za kiislam.
Wanahabari wakiwa katika hafla hiyo
Uzinduzi wa huduma hiyo umekwenda sambamba na uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa mteja ambapo bank hiyo imeanza kuadhimisha wiki hiyo leo ikiwa ni kuendelea kusherekea miaka Mitano ya Bank hiyo tangu ianze kutoa huduma za kibenk nchini Tanzania.

No comments: