Tuesday, November 1, 2016

HAKUNA SHAKA TUMEJIANDAA-MBEYA CITY FC


dsc_0102KOCHA  Mkuu wa Mbeya City  Fc, Kinnah Phiri amesema ameajindaa vizuri  ‘kuikabili’ Young Africans  kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara   uliopangwa kuchezwa kesho jumatano kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Muda mfupi uliopita Kocha Phiri ameiambia mbeyacityfc.com kuwa anaamini utakuwa mchezo mzuri na mgumu kwa sababu timu zote mbili zimetoka kushinda mechi zake zilizopita huku akiahidi ‘kuiduwaza’ Yanga kwa kipigo kutokana na maandalizi  mazuri aliyoyafanya kwa kikosi chache na kutupilia mbali hofu yoyote kutoka kwa timu hiyo akiamaini timu zote hizi mbili zina mchezo sawa.
“Kweli,kesho tunacheza na Yanga, utakuwa mchezo mzuri kwa sababu timu zote zimeshinda michezo iliyopita,sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda,hatuna shaka yoyote kwa sababu timu zote zina mchezo sawa, jambo jema ni maandalizi tuliyoyafanya na sapoti ambayo tutaipata kutoka kwa mashabiki wetu,watu waje uwanjani na wajiandae kushangaa kile kitakachofanywa na timu yangu”alisema.

Akiendelea zaidi kocha huyo raia wa Malawi alisema kuwa City imebakiza michezo miwili, wa kesho na ule wa tarehe 7 dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Manungu Turiani  hivyo anachokitizama sasa ni kushinda michezo hii miwili ili kuweza kupata pointi 6 ambazo  zitaicha timu City   kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi kabla ya kukamilika kwa duru ya kwanza.
“Tumebakiwa na michezo miwili, wa kesho na ule ambao tucheza dhidi ya Mtibwa, tuko kwenye nafasi ya tisa sasa, lengo letu ni kushinda michezo hii ilikuweka mazingira mazuri katika msimamo wa ligi kabla hatujamaliza duru ya kwanza, hii ina maana kuwa tutakapo rejea kuanza duru ya pili tutacheza kwa nguvu kutafuta nafasi mbili za juu” alimaliza.

No comments: