Monday, November 7, 2016

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe 4 Novemba 2016

Mauzo ya Soko
Idadi ya mauzo imeongezeka kwa asilimia 56% na kufikia TZS 8.3 Bilioni kutoka TZS 5.3 Bilioni wiki iliyopita.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imeongezeka mara mbili (x2) hadi 1.8 Milioni kutoka 869,453 wiki iliyopita.

Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     SWISSPORT kwa asilimia 45.20%
2.     DSE kwa asilimia 39.64%
3.     TBL kwa asilimia 11.49%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa asilimia 0.4% na kufika Trilioni 21.9 kutoka Trilioni 21.8 wiki iliyopita.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia umepanda kwa asilimia 0.3% hadi Trilioni 8.21 kutoka Trilioni 8.19 wiki iliyopita.

Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda imejitokeza wiki hii kuongezeka Zaidi ya pointi 52 baada ya bei ya hisa za TBL kuongezeka kwa asilimia 1.5%.

Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha wiki hii imeongezeka kwa pointi 2.6 baada ya bei ya hisa za DSE kuongezeka kwa asilimia 8%.

Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii imeshuka kwa pointi 376 kutokana na bei ya hisa za SWISSPORT kushuka kwa asilimia 14%.

No comments: