Monday, November 14, 2016

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe 11 Novemba 2016



Mauzo ya Soko
Idadi ya mauzo imepungua kwa asilimia 23% na kufikia TZS 6.4 Bilioni kutoka TZS 8.3 Bilioni wiki iliyopita.
Ingawa Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeongezeka mara sita (x6) hadi 11 Milioni kutoka 1.8 Milioni wiki iliyopita.

Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     CRDB kwa asilimia 95.45%
2.     TBL kwa asilimia 2.18%
3.     DSE kwa asilimia 1.44%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa wastani wa asilimia 2.1% hadi Trilioni 21.4 kutoka Trilioni 21.9 wiki iliyopita.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia umepungua kwa wastani wa asilimia 0.3% hadi Trilioni 8.19 kutoka Trilioni 8.21 wiki iliyopita.


Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda imejitokeza wiki hii kupungua kwa wastani wa pointi 17.7 baada ya bei ya hisa za TCC kupungua kwa asilimia 1.7%.

Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha wiki hii imepungua pointi 4.5 baada ya bei ya hisa za DSE kushuka kwa asilimia 6%.

Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 3,157 sawa na wiki iliyopita.

Ingawa idadi ya mauzo ilishuka pamoja na ukubwa wa mtaji, mabadiliko haya ni ya wastani na yanatokana zaidi na shughuli za uuzaji na ununuzi wa hisa. Muhimu zaidi ni kwamba nguvu za soko za uhitaji (demand) na uwepo (supply) wa hisa zinachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya ukubwa wa mtaji wa soko kwa ujumla. 

No comments: