Monday, November 21, 2016

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe 18 Novemba 2016

Mauzo ya Soko
Idadi ya mauzo imeshuka kwa asilimia 37% na kufikia TZS 4 Bilioni kutoka TZS 6.4 Bilioni wiki iliyopita.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imeshuka kwa asilimia (94%) hadi laki 671,618 kutoka Milioni 11,065,589 wiki iliyopita.

Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     CRDB kwa asilimia 42.40%
2.     TBL kwa asilimia 41.44%
3.     DSE kwa asilimia 6.44%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 2.4% na kufika Trilioni 20.9 kutoka Trilioni 21.4 wiki iliyopita.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia umeshuka kwa wastani wa asilimia 0.6% hadi Trilioni 8.14 kutoka Trilioni 8.19 wiki iliyopita.

Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda imejitokeza wiki hii kupungua kwa pointi 40.84 baada ya bei ya hisa za TCCL na TBL kupungua kwa asilimia 13.98% na 0.74%.

Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha wiki hii ilibaki kwenye wastani ule ule wa Tzs 2,771.18.

Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii ilibaki kwenye wastani ule ule wa Tzs 3,157.95.

No comments: