KINGAMUZI CHA ZUKU SASA WAMEKULETEA ZUKU SWAHILI MOVIES

Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Omari Zuberi akizungumza na wanahabari na wadau wa filamu wakati wakitangaza kuanzishwa kwa Zuku Swahili Movies Jijini Dar es salaam leo

 Sinema za kitanzania yaani Bongowood zimepata umaarufu mkubwa na kuonyeshwa kwa asilimia kubwa kwenye TV za Afrika Mashariki kunapozungumzwa Kiswahili na pote barani Afrika.

Kwa kuliona hilo Kampuni ya Visembuzi aina ya ZUKU waliamua kuanzisha huduma ya kuwafikishia wateja kazi zinazofanywa na kuwezesha sekta ya sanaa kukua zaidi kupitia Chanel yao ya Zuku Swahili Movies ambapo inazinduliwa upya Novemba 13, kwa jina la Zuku Swahili huku ikiwa na maboresho zaidi.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu nchini Saimon Mwakifamba alikuwepo katika Mkutano huo
Akizungumza mbele ya Wanahabari Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Omari Zuberi amesema kuwa kutokana na fursa ya ukuaji wa Bongowood, Zuku Tv iliwekeza na kuzindua Zuku Swahili movies mwaka 2013, iliyotengenezwa kwa ajili ya sekta ya Filamu Tanzania.


Ameongeza kuwa Zuku Channel 210 sasa itakuwa na burudani bora zaidi kutoka bongo muvi, na vipindi vingine vyenye mlengo wa Burudani zaidi.

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu nchini Saimon Mwakifamba amewataka Zuku kuboresha maslahi zaidi kwa wasanii hususani waandaaji wa Filamu na sio madalali wa Filamu hizo kwani kumekuwa na Kesi nyingi za wizi wa kazi za wasanii.

Afisa Mahusiano kutoka Bodi ya Filamu nchini Tanzania ABUU KIMARIO akisisitiza jambo katika mkutano huo

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.