Tarehe
13.11.2016 saa 09:30 usiku huko maeneo ya Tuwangoma mtaa wa msaki Mbagala,
Kikosi Maalum cha Kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalum
ya Dar Es Salaam kilifanikiwa kuwakamata majambazi watano baada ya kupatikana na mali
ya wizi ambayo iliporwa kwa nguvu nyumbani kwa
PATRICK SAMARI miaka 35, mfanyakazi wa mamalaka ya bandari kitengo cha
biashara, mkazi wa Tuwangoma ambaye alivamiwa na kundi la majambazi wapatao 15 nyumbani kwake.
Majambazi
hao walikuvunja mlango kwa matofali na kufanikiwa kuingia ndani na kuiba vitu
vifuatavyo;
Bastola
yenye usajili A731441 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine yake, kiasi cha
fedha Tzs 10,180,0000/= milioni kumi na laki moja na elfu themanini, Flat
Screen Tv 2 ‘54’ Laptop mbili aina ya HP, simu mbili za mkononi aina ya Samsung
Baada
ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa
PATRICK SAMARI, kikosi kazi kilianza kazi ya ufuatiliaji tarehe 14.11.016
walikamatwa watuhumiwa wafuatao;
1.PENZA
SELEMAN. 2 MWARAMI NASOTO. 3 SWEED SHABANI, miaka 40, mkazi wa kinondoni
Manyanya 4 MUSSA ISMAIL miaka 27,
dereva, mkazi wa Sinza na 5.SALUM
TAIDINI.
Watuhumiwa
wote hao walikiri kuhusika na tukio hilo na mali zote za wizi walidai
walihifadhi kwa SALUM TADINI, baada ya mahojiano zaidi na upekuzi vilipatikana
vifaa vyote vilivyoibiwa kama ifuatavyo;
1.Gari
T533 DEQ aina ya Toyota TI inayotumika
kubebea mizigo sehemu wanazoiba.
2.Televisheni
4 aina ya Samsung
3.Laptop
mbili
4.Remote
control mbili
5.External
driver moja.
6.Subwoofer
moja
7.Deck
moja
8.King’amuzi
kimoja
9.Simu
2
10.Remote
Aidha
katika tukio hili watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kuonyesha Bastola waliyoiiba na kuweza kubaini
matukio mengine waliyowahi kushiriki au kutenda katika maeneo mbalimbali
jijini Dsm. Upelelezi wa tukio hili
unaendelea utakapokamilika watuhumiwa watapelekwa mahakamani kujibu mashtaka
yanayowakabili.
HABARI NYINGINE KUTOKA POLISI ZIPO HAPO CHINI
KUKAMATWA KWA WANAWAKE 4 NA WATOTO
4 WANAOFUNDISHWA UHALIFU WA KUTUMIA
SILAHA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kupitia
kikosi kazi kinachopambana na uhalifu wa kutumia silaha na ujambazi, kimefanikiwa kukamata wanawake wanne na watoto
wanne waliokuwa wamefichwa kwenye kambi. Mafanikio hayo yalipatikana baada ya
kikosi kazi kufanya oparesheni kali katika maeneo mbalimbali ya misitu ya pori la VIKINDU. watoto hao wanne waliokuwa wametoroshwa katika
familia ya ABDALA MALECK
Aidha
Polisi ilipokea taarifa toka kwa mzazi mmoja wa kiume aitwaye SHABANI ABDALA
MALECK mkazi wa kitunda kuwa ametoroshewa watoto wanne na mtalaka wake aitwaye
SALMA MOHAMED, aliyeingizwa kwenye harakati za kigaidi.
Jitihada
za pamoja na kati ya mtoa taarifa na Polisi zilifanikisha kuwakamata wanawake
wanne na watoto wanne katika eneo la Kilongoni VIKINDU mkoa wa Pwani wakiwa
wamekusanywa kwenye nyumba ya mtu mmoja anayeitwa SULEIMAN, wakiwa wanafundishwa mambo ya dini
na harakati za kigaidi.
Watoto
hao ni 1.AISHA SHABAN miaka 13, mwanafunzi darasa la saba shule ya msingi
Kizange kitunda.
2.ASHA
SHABANI miaka 8, mwanafunzi darasa la nne, shule ya msingi Jitihada kitunda.
3.ABDURAHAMAN
SHABANI miaka 8, mwanafunzi dara la nne, shule ya msingi Jitihada kitunda
4.FATUMA
SHABANI miaka 2, mtoto wa nyumbani.
Baada
ya mahojiano zaidi imeijidhihirisha kuwa wengi wao wameachishwa masomo
katika shule mbalimbali hapa
nchini.baadhi ya watoto wameachishwa na wazazi /walezi wao na kuingizwa katika
madrasa ambazo ndizo kambi walikokamatiwa chini ya uangalizi wa wanawake
waliokamatwa pamoja nao. Sambamba na mafunzo ya madrasa pia wamekuwa
wakifundishwa ukakamavu(karate/kumfuu/judo) na silaha aina ya SMG na bastola,
pia wanafundishwa kupiga maeneo tete ya kummaliza mtu pumzi na kufariki haraka
wakati wa mapigano (pressure point)ili kumdhibiti adui, kulenga shabaha kwa
kutumia risasi, kutumia kitako cha bunduki na singe. Watoto hao wamefundishwa
kuwa adui yao mkubwa ni Polisi, walinzi katika taasisi za fedha na makafri
katikakujipatia kipato, wamefunzwa kupora au kunyang’anya kwa kutumia silaha na
kutumia viungo
vyao.
Wanawake
hao na watoto wanaendelea kushikiliwa kwa ajili ya mahojiano ili kuweza kubaini
mtandao mzima katika suala hili ili kutokomeza tabia hii ya kuwachisha watoto
wadogo shule na kuwaingiza katika vitendo vya uhalifu.
KUKAMATWA KWA MAGARI 4 YALIYOIBWA NA WATUHUMIWA 4
Tarehe
10.11.2016 kikosi kazi cha Polisi kanda
maalum cha kuzuia wizi magari kilifanikiwa kukamata gari T616 DCH Toyota
L/cruiser mali ya JOSEPH KAYAWAYA iliyoripotiwa kuibiwa Dsm na nyaraka kughushiwa na ikauzwa jijini
Arusha, kikosi kazi kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa DEMESTRIOUS APOLINARY
padri wa kanisa katoliki Sumbawanga.
Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa
mahakamani.
Katika
tukio la pili Polisi walipokea taarifa za kuibiwa magari mawili moja aina ya
SCANIA T511 AWB mali ya NELSON DANIEL mkazi wa keko juu iliibiwa keko akiwa
amepaki na kupatikana Tabata na gari namba T814 DEF Mitsubish Canter mali ya
HOSEA KAPULA gari hii iliibiwa sehemu isiyojulikana na mlalamikaji aligundua
baada ya kununua kupewa nyaraka bandia, gari hilo lilikamatwa jijini DSM maeneo
ya kigamboni.
Watuhumiwa
waliokamatwa katika matukio haya mawili ni kama ifuatavyo;
1.AMANI
DICKSON miaka 23, mkazi wa kigamboni
2.EXAUD
MARTIN miaka 40, mkazi wa nikocheni
3.RASHID
HARUNA miaka 28, mkazi wa magomeni
4.MZEE
NASSIBU miaka 41, mkazi wa Yombo
Tukio
lingine Polisi kupitia kikosi kazi chake kilipokea taarifa za unyang’anyi wa
kutumia nguvu toka kwa HASHIM ALLY mkazi
wa kibamba kuwa ameibiwa gari lake T 724 DHZ Isuzu Canter rangi nyeusi baada ya kukodiwa kwenda kubeba
jenereta maeneo ya kibwegere na kijana
anayemfahamu kwa sura, ndipo walipofika eneo la tukio wakati akigeuza gari ili
apakie mzigo huo alikabwa na vijana wapatao watatu na kumfunga kamba na kumtupa
kisha kuondoka na gari. Mtuhumiwa alifanikiwa kufungua kamba na kuomba polisi
na Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja na wengine walikimbia
kusikojulikana na kutelekeza gari hilo maeneo ya Bunju A. Mtuhumiwa huyo ni
RAJABU ALLY miaka 35 fundi magari, mkazi wa Bunju A. mtuhumiwa anaendelea
kuhojiwa mara upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani.
POLISI
KANDA MAALUM DSM WAMEKUSANYA TSH 587,520, 000 /= KUPITIA TOZO ZA MAKOSA YA
USALAMA BARABARANI
Jeshi
la Polisi Kanda maalum DSM kupitia Kikosi chake cha Usalama barabarani
kimekamata makosa mbalimbali ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia
tarehe 09.11.2016 hadi tarehe 16.11.2016 na kuingizia serikali mapato ya ndani
kama ifuatavyo;
1.
Idadi ya magari yaliyokamatwa - 18,073
|
2.
Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa - 1,511
|
3.
Daladala zilizokamatwa - 6,113
|
4.
Magari mengine (binafsi na malori)
- 11,960
|
5.
Bodaboda waliofikishwa
Mahakamani -
|
kwa makosa ya kutovaa helmet na
|
kupakia mishkaki -
|
6.
Jumla ya Makosa yaliyokamatwa -
19,584
|
Jumla
ya Fedha za Tozo zilizopatikana Tzs
587,520,000/=.
Madereva wote wanatakiwa kutii sheria
za usalama barabarani na washirikiane na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa juu
ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani ili kudhibiti matukio ya ajali
zinazoweza kuzuilika.
POLISI
NA TRA WAFANIKIWA KUTEGUA MBINU MPYA YA WAKWEPA KODI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm kwa
kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania imefanikiwa kubaini mbinu mpya
inayotumika na wakazi wa Mbweni ili kufanikiwa katika kupitisha bidhaa
zisizolipiwa ushuru.
Aidha Polisi wakiwa pamoja na mamlaka
ya Mapato Tanzania huko maeneo ya Mbweni katika njia wanazotumia kupitisha
bidhaa zilizokwepa kulipiwa ushuru wanatega mbao zenye misumari, nia yao ni kuharibu magari ya doria kwa
kutandika mbao hizo chini ya barabara ili magari yapate pancha na kushindwa
kuwafuatilia.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ametoa
onyo kali kwa wananchi wa maeneo hayo operesheni kali inaendelea ili kuwakamata
wote wanaofanya vitendo hivyo na sheria itachukua mkondo wake.
S.N.SIRRO - CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA
MAALUM
DAR ES
SALAAM
No comments:
Post a Comment