Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole,Dk. Augustine Mrema akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) , Jijini Dar es Salaam leo. |
MWENYEKITI
wa Taifa wa Bodi ya Parole, Dkt. Augustine Mrema amemwandikia barua
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango
wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na wasamaria wema
baada ya kukidhi vigezo.
Dkt.
Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa kutoa taarifa yake hiyo kwa waandishi
wa Habari Jijini Dar es Salaam kuzungumzia suala lake hilo la Maafisa wa
Magereza kusitisha hatua ya kukatisha mpango wake licha ya kuwalipia wafungwa
waliokidhi vigezo.
“Mimi nimeona nisinyamaze,napaza sauti nataka Rais aone, ajue kama
magereza yetu yanashida na tunalotatizo kwa nini mpango huu umesimamishwa na
umesitishwa tumekosea wapi?. Nimesha muandikia barua Waziri Mkuu kulalamikia
jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari tumesha walipia faini
hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya kosa lipi? Ama Mama
Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha zoezi hili” amesema
Mrema kwa waandishi wa habari.
Hata
hivyo Mtandao huu ulipohoji juu ya kama fedha zilizolipwa za Mchungaji Mama
Rwakatare zinaweza kurejeshwa ama la!, Mrema amesema kuwa suala hilo lipo chini
ya Mama Rwakatare mwenyewe ila wanasubiria hatua kutoka kwa Rais na Waziri Mkuu
ambapo wameshatoa malalamiko yao juu ya suala hilo.
Dk
Mrema amewaonyesha wandishi wa habari nyaraka ikiwemo risiti mbalimbali
walizofanya malipo kwa ajili ya kuwatoa wafungwa hao ambapo amesema haki ya
kuzuia mpango huo imeweza kumuumiza vibaya kwani wasamaria wema walioweza
kujitolea fedha za mpango huo imewagusa pia.
Pia
ameongeza kuwa, mpaka sasa magereza mbalimbali kuna msongamano wa
wafungwa ambao wanahitaji msaada wa kutoka ila hawajapata fedha za kulipiwa
hivyo pindi wasamalia wema kama Mchungaji Mama Rwakatare wanapojitokeza
wanatakiwa kupongeza na wala si kupinda kona kona.
Hivi
karibuni Jeshi la Magereza lilisitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na
Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi
hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.
Awali
ilidaiwa kuwa Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti
wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78
kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni.
Kwa
mujibu taarifa zilizonukuliwa katika moja ya vyombo vya habari hapa mchini
vilieleza kuwa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema
amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi
hilo na kuongeza kuwa, wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini
hiyo ndugu zao.
Hata
hivyo Mrema amesema mpango huo ulilenga kupunguza msongamano wa wafungwa
magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hivyo
usitishwaji huo unalenga kurudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo katika
kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo.
CREDIT --MWANGALA BLOG
No comments:
Post a Comment