POLISI DSM YAKAMATA BASTOLA NNE, BROWNING 01, REVOLVER 02, GLOCK 19 MILIPUKO 06 NA RISASI 16

Tarehe 16/11/2016 saa 10:00 jioni huko Mbande Mbagala, askari wa kikosi maalumu cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kimefanikiwa kumkamata jambazi aitwaye KURWA RAJABU@MAMBA akiwa na
 silaha aina ya “BROWNING” yenye namba A731441 ikiwa na risasi (12) ndani ya magazine, baada ya kuwekea mtego.

Silaha hiyo iliibiwa Tarehe 13.11.2016 saa 09:30 usiku huko maeneo ya Tuwangoma mtaa wa Msaki Mbagala katika tukio la uvunjaji na kuibwa kwa vifaa mbalimbali ambavyo vyote vilipatikana kwa juhudi za ufuatiliaji wa makachero wa Polisi. Aidha baada ya mahojiano ya kina jambazi alitaja silaha nyingine ambayo ni  bastola aina ya REVOLVER iliyofutwa namba ikiwa na risasi mbili ikiwa imefichwa maeneo ya msitu wa DONA  huko Yombo.

Katika tukio lingine tarehe 16/11/2016 kikosi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha kilipata taarifa kuwa kuna jambazi aitwaye SHOMALI anayetafutwa KWA MAUAJI yaliyofanyika kwenye daladala tarehe 28/10/2016 huko Tandika Tambuka reli  kuwa ameonekana huko Tandika Maguruwe akiwa amekaa nje ya saloon na wananchi wameingiwa hofu pamoja na woga.


 Polisi wa kikosi kazi walipofika eneo hilo jambazi huyo alianza kukimbia na ndipo askari walifyatua risasi juu ili asimame lakini hakutii amri askari walimpiga risasi mbili mguuni na kudondoka chini kisha kumkamata pamoja na bastola yake aina ya REVOLVER ikiwa na risasi mbili ndani ya magazine, mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.