Simu hizo za THURAYA zinazotumia mawasiliano ya Satellite |
Hii
inaweza kuwa ya kwanza kutokea kwa Tanzania katika kumbukumbu za maswala ya
mawasiliano hususani ya simu za mkononi ambapo Jana Jijini Dar es salaam imezinduliwa
Simu ya aina yake ambayo tofauti na simu za kawaida simu Hii inatumia
Mawasiliano ya njia ya SATELLITE ambayo ni tofauti na simu nyingine ambazo
zinatumika nchini kwa sasa ambazo zinatumia Mtandao wa njia ya kawaida wenye
minara ya Baharini.
THURAYA
XT-PRO ni moja kati ya simu Bora sana Duniani kwa sasa zinazotumia Satellite
ambayo pia inasifika kuwa na uwezo mkubwa wa Vifaa vyake kama Battery,na uwezo
mkubwa wa Mtandao bila kujali eneo ulilopo kote duniani,sifa nyingine kwa simu
hiyo ni pamoja na kuwa na Kioo imara cha simu yake chenye uwezo wa kuhimili
mikikimikiki ya aina yoyote
Wadau Mbalimbali wakikagua simu aina ya Thuraya ambazo zimezinduliwa Jana Jijini Dar es salaam |
Katika
uzinduzi wa Thuraya XT-PRO Jana Jijini Dar es salaam Meneja Mauzo wa kampuni
hiyo kwa Africa Augustus Kamitu amesema
kuwa kupitia simu za Thuraya XT-PRO mtumiaji atakuwa na uwezo wa Kupiga simu na
kupokea simu pamoja na kutuma messege kwa kutumia Satellite ikiwa ni pamoja pia
na kutumia mtandao kufanya shughuli mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii
kwa Kutumia Mtandao wa satellite.
Ameongeza
kuwa ubora wa Thuraya unajidhihirisha zaidi pale ambapo ukiwa na simu hiyo
hutakuwa na hofu ya eneo ulilopo kwani simu hizo zina uwezo wa kuhimili mtandao
eneo lolote ulilopo bila kuwa na usumbufu wa mtandao
Simu
hizo kwa sasa zinapatikana zaidi ya mataifa 160 ya dunia nzima ikiwemo
Ulaya,Asia,Africa na Australia
ambapo kwa Tanzania
imezinduliwa Jana Jijini Dar es salaam na kwa sasa inaoatikana.
No comments:
Post a Comment