Friday, November 11, 2016

TAIFA STARS YAONDOKA MCHANA HUU NOVEMBA 11, 2016

Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro kutoka Kampuni ya Bia Tanzania inatarajiwa kuondoka leo Ijumaa saa 7.15 mchana Novemba 11, mwaka huu kwenda Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ni: Makipa  Deogratius Munishi na Aishi Manula, Mabeki ni Erasto Nyoni Michael Aidan, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein na Vicent Andrew.
Viungo wa Kati ni Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Jonas Mkude na Muzamiru Yassin na wale wa pembeni ni ni Shiza Kichuya, Simon Msuva na Jamal Mnyate na washambuluaji ni Ibrahim Ajib, John Bocco, Mbwana Samatta, Elius Maguli, Thomas Ulimwengu na Omar Mponda     .
Mchezo huu utakuwa na faida zaidi kwa Tanzania kama ikiwafunga Wazimbabwe kwa kuwa itaongeza alama za nyongeza kwa kushinda ugenini.
Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 144 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Zimbambwe yenyewe inashika nafasi ya 110.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Chile, Colombia na Ujerumani.
Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 31 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Senegal (32), Algeria (35), Tunisia (38) na Ghana (45)

No comments: