Commissioner General Tanzania Insuarance Regulatory authority and Board chairman Israel Kamuzora akizungumza katika mkunao huo wa wanahabari. |
Mwenyekiti wa wa wakala wa umeme Vijijini Dr Gideon Kaunda akizungumzia umuhimu wa jukwaa hilo ambalo limekutana Jijini Dar es salaam |
Katika mkutano wa waandishi wa habari leo Wakala wa Bima ya Biashara Afrika
(ATI) umeitaka serikali ya Tanzania
kuimarisha ushirikiano uliopo baina yake
hivi sasa ambao utawezesha wakala huyo
kuingia uwekezaji mkubwa wa dola
za Marekani bilioni 1.2 (2.6tr/-) katika sekta ya nishati pamoja na nyongeza ya megawati 1,200 katika
gridi ya taifa.
Tanzania ni mmoja wa
wajumbe waliasisi ATI wakala ambao ulianzishwa ili kutoa bima kwa wawekezaji pamoja na kufanya shughuli nyingine za kibiashara
miongoni mwa nchi za Afrika ambazo ni wanachama. Chini ya ubia am,bao
ulisainiwa na Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamini William Mkapa mwaka 2001,
Tanzania na nchi nyingine zilikubaliana kutoa upendeleo wa kupata mkopo katika miradi yote inayoungwea mkono na ATI. Ahadi hiyo ambayo inatoa
uhakika kwa nchi mwanachama ambao
utaiepusha na madai yoyote katika miradi
inayoungwa mkono na ATI, kuwapatia wawekezaji, wagavi na na nafasi nyingine muhimu katika kuzindua
miradi Tanzania.
“Lengo letu ni kuisaidia
Tanzania kwa kuuleta nchini
uwekezaji unaohitajika sana na kupunguza
gharama za kukopa. Sisi ni watu wakimya
lakini ni sehemu muhimu sana ya fumbo
kwa sababu tumesimama nyuma ya uwekezaji na biashara ambayo inakadiriwa kufikia dola bilioni (2tr/-)
nchini Tanzania tangu kuanza kwa biashara mwaka 2004”, alibainisha Ofisa
Mtendaji Mkuu wa ATI George Otieno.
Tanzania inaweza kunufaika
zaidi kutokana na ubia wake na ATI kirahisi kwa kurudia utekelezaji wa ahadi
zake kwa kusaidia miradi inayoungwa mkono na ATI ndani ya Tanzania.
Chini ya masharti ya ubia, Tanzania
inaweza kuwepo kiwango mbadala wa
vipimo vya viwango kwa kipimo cha uwekezaji cha ATI daraja A mara tutakaposaini manunuzi yanayoungwa mkono na ATI. Chini ya kanuni
za Basel, ambazo zinasimamia mabenki mengi ya kimataifa, ynaweza kuikopesha
nchi kama Tanzania ikiwa inaungwa mkono katika bima na taasisi
kama ATI, ambayo ni taasisi
inayoheshimika na inayoaminiwa na masoko
ya kimataifa ya fedha. Bima ya ATI
inaiwezesha benki kupunguza kiwango cha mwisho cha malipo ya bima,
ambacho kwa kiwango kikubwa kinapunguza
gharama za kukopa kwa Tanznaia na nchi nyingine za Afrika ambazo ni
wanachama.
Kushindwa kutumia
kikamilifu fursa hii, Tanzania inaweza
kukosa uwekeza wenye thamani ya
mamilioni ya fedha. “ATI inaweza
kuisaidia nchi kuwa inavutia kuwekeza kifedha
kwa kuvutia uwekezaji zaidi. Hili ni muhimu hususani katika sekta ya
nishati ambayo kwa hivi sasa ina
ushindani mkubwa,” alisema Mdhamini Mkazi wa ATI nchini Tanzania Tusekile Kibonde.
Mkutano huo wa waqandishi
wa habari umefanyika wakati mkutano wa
jukwaa la kimataifa la sekta ya nishati
ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji kutawezesha ongezeko kubwa la
Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na ATI. Jukwaa hilo linawakutanisha pamoja
wadau kutoka Nyanja binafasi za za umma
katika kutafuta masuluhisho
ambayo yataondoa hatari
zinazoikabili sekta ya nishati ili kuvutia uwekezaji unaohitajika sana.
Wakala wa Bima ya Biashara
Afrika (ATI) ulianzisha zaidi ya mwongo mmoja uliopita na Tanzania na nchi nyingine wanachama wa
Soko la Pamoja na nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA), Benki ya Dunia (WB), na
Benki ya hivi karibuni ya Maendeleo Afrika (ADB) ili kusaidia kuvutia uwekezaji kutoka nje (FDI) na
kusaidia biashara. ATI inashughulikia masuala yanayowahusu wawekezaji kwa
kuzipatia bima biashara zao dhidi
ya majanga mbalimbali za kiuwekezaji
kama vile kushindwa kuilipa serikali au wakala wa serikali. Hali
kadhalika ATI inazilinda kampuni za ndani
zinazovutiwa katika kupanua
biashara zao ndani ya masoko mapya. ATI
ilianzishwa uwepo katika maqzingira ya ndani nchini Tanzania mwaka 2010.
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)
ndio mwenyeji wake katika ofisi yake ya Tanzania.
Nchini Tanzania ATI
inaunga mkono sekta binafsi na serikali
katika kushughulikia changamoto katika
nishati, mawasiliano ya simu na huduma
za kifedha. Katika sekta ya nishati ATI inaisaidia kampuni ya Norway ambayo imepewa ukandarasi na
serikali katika kujenga vituo vya umeme
na hali kadhalika kiasi cha dola milioni
62 (132bn/-) kwa ajili ya kuwezesha kujengwa
kwa kuanzisha ushirika na mabenki
kwa ajili ya matumizi ya serikali. Kutokan ana uungwaji mkono huo wa ATI
katika miradi kama hiyo , Tanzania
imeweza kuingiza mega wati 400 za umeme
za ziada katika gridi ya taifa.
No comments:
Post a Comment