Vijana wa ACT-WAZALENDO wamlilia Samweli Sitta


NGOME YA VIJANA TAIFA ACT WAZALENDO

Kwa majonzi makubwa tunaungana na kutoa pole kwa Chama Cha Mapinduzi,Familia na Taifa kwa ujumla kwa kumpoteza Spika Mstaafu Wa Bunge La Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa John Samwel Sitta aliyefariki mnamo tarehe 7 Novemba,2016.
Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa hii kwani Samwel John Sitta alikuwa ni Kiongozi na Spika Wa Bunge ambaye aliitendea haki nafasi yake na kuitendea haki Nchi Ya Tanzania katika kipindi chake.
Ni katika bunge la Spika Wa Bunge Samwel John Sitta Watanzania tuliona maana halisi ya bunge na nguvu ya bunge kwa serikali na wananchi wake kwa ujumla.
Demokrasia ilishika mkondo wake,maslahi ya Nchi yalikuwa ndio kipaumbele na uwajibikaji ulifanyika kwa vitendo bila kumung'unya isipokuwa kwa uhalisia wake.
Hakika tumepoteza mtu muhimu sana katika Taifa Letu la Tanzania ambaye alikuwa ni mfano wa kuigwa na kamwe pengo lake halitakuwa rahisi kuzibika.
Kama vijana wa chama cha ACT Wazalendo pamoja na vijana wengine wote wa Taifa letu la Tanzania tutakuenzi mzee wetu.
Eeh Mwenyezi Mungu,mwingi wa rehema uiweke roho ya Mzee wetu Samwel John Sitta mahali pema peponi ameni.
Edna Sunga
Katibu Vijana Taifa ACT WAZALENDO
8 Novemba,2016.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.