Monday, November 14, 2016

WASAIDIZI WA KISHERIA WA SHIRIKA LA EfG WAUNGA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KATIKA KUFANYA USAFI

Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye (kushoto), akiwaongoza kufanya usafi Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli katika suala zima la usafi wa mazingira.

Msaidizi wa kisheria katika soko hilo, Batuli Mkumbukwa 
akifanya usafi.
Wasaidizi wa kisheria wakiwa kazini. Kutoka kushoto ni Aisha Juma kutoka Soko la Tabata Muslim, Mashimi Mbogela na Irene Daniel.
Mifagio ikipigishwa kwata ya usafi.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye (kushoto) na Charles Beatus wakifanya usafi.
Usafi ukiendelea.
Makamu Mwenyekiti wa Soko hilo, Issa Ndilima (kulia), akishiriki kufanya usafi. Kushoto ni Kashinde Kapambale na Aisha Juma kutoka soko la Muslim
Msaidizi wa sheria kutoka Soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala, Charles Beatus (kushoto), akitoa somo kwa wafanyabiashara wa soko hilo kuhusu ukatili wa kijinsia.
Shughuli za usafi zikiendelea.
Hapa kazi tu.
Takataka zikiondolewa sokoni hapo baada ya kufanyika usafi.


Na Dotto Mwaibale

WASAIDIZI wa kisheria wanawake kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), wamemuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika uhimizaji wa kufanya usafi Soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki sokoni hapo Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa EFG, Shaban Rulimbiye alisema wameamua kufanya usafi wa mazingira katika masoko sita yaliyopo chini ya mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia masoko unaoendeshwa na shirika hilo.

"Tunamuunga mkono rais wetu kwa jitihada zake anazozifanya za kuhimiza usafi ndio maana wasaidizi wetu wa kisheria kutoka katika masoko hayo tupo nao hapa Temeke kufanya usafi na baada ya hapo watatoa elimu kwa wafanyabiashara ya kupinga ukatili huo " alisema Rulimbiye.

 Alisema ukatili wa kijinsia masokoni si kumshika maungoni mfanyabiasha na matusi hata pale wanawake wanapofanya biashara zao kwa kuziweka chini bila ya kuwa katika mazingira mazuri pia ni ukatili wa kijinsia.

Alisema mpango huo wa kufanya usafi katika masoko hayo ni endelevu na kuwa kila Jumamosi watakuwa wakifanya hivyo kumuunga mkono rais.

Rulimbiye aliyataja masoko ambayo yapo chini ya mradi huo ambayo yatanufaika na usafi huo wa mazingira kuwa ni Temeke Stereo, Mchikichini, Kisutu, Feri, Gezaulole na Tabata Muslim.

Makamu Mwenyekiti wa soko la Temeke Sterio, Issa Ndilima alilishukuru shirika hilo kwa mpango huo wa usafi kwani umeleta hamasa kwa wafanyabiashara wa soko hasa katika mafunzo wanayopata kupitia wasaidizi wa kisheria kupinga ukati wa kijinsia masokoni.


No comments: