Jeshi la Polisi kanda maalumu Dar es salaam
linaendelea na oparesheni mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya jiji na
kufanikiwa kukamata watuhumiwa jumla ya watuhumiwa 67 kati yao watuhumiwa watano walikamatwa kwa
makosa ya kuuza na kusambaza pombe bandia aina ya konyagi na vifaa vya
kutengenezea kinywaji hicho kama ifuatavyo;
1.Chupa tupu za konyagi 175.(2.) Chupa zenye kinywaji cha konyagi 17. (3.) Vifungashio vya viroba vya konyagi 111. (4.) Vifuniko vya chupa za
konyagi 200. (5.) Lebo na stika za
konyagi.(6.) Katoni 111 za viroba
vya konyagi. (7.) Vimiminika vya
pombe aina ya spiriti lita 20. (8.) Ndoo
kubwa aina ya jaba moja na koki 10 .(9.)
Viroba original pakiti 14,916 (10.)Victorious
pakiti 1,080.
Watuhumiwa
waliokamatwa na bidhaa hizo bandia ni kama ifuatavyo;
1.LADNESS
GRATION KAGARUKI miaka 26, mkazi wa sinza madukani
2.ALOYCE
EMMANUEL miaka 53, mkazi wa Salasala
3.LEORNAD
AROBOGASTI miaka 49, mkazi wa Makongo.
4.GODFREY
GABRIEL miaka 29, mkazi wa Mwenge.
5.AVELINE
SANDOLE miaka 58, mkazi wa Mwenge.
Watuhumiwa
wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani
kujibu mashtaka yanayowakabili.
Habari Nyingine Kutoka Polisi zipo chini-----------
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WAWILI WA UNYANG’ANYI WA
KUTUMIA NGUVU
Tarehe
20/11/2016 saa 09.00 jioni huko kariakoo mtaa wa mkunguni na sukuma Polisi
ilipokea taarifa toka kwa SAHIM MOHAMED (24), kwamba meneja masoko wa kampuni ya DISCOUNT
CENTRE akiwa nyumbani kwake jengo la ghorofa 07, alivamiwa na watu wawili
wakiwa na silaha za jadi.
Polisi
baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kuwawahi watuhumiwa RAMADHANI ABDI (42) mkazi wa jangwani na
AMIRI ALLY (50), mkazi wa Tabata. Watuhumiwa walikamatwa na vifaa mbalimbali
walivyoiba kabla hawajaondoka eneo la tukio na vifaa hivyo ni laptop 01, ipad 01, pesa taslim Tsh 120,000/= na silaha walizotumia kuiba ni visu, bisibisi na kipande
cha nondo.
watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na baada
ya upelelezi kukamilika watapelekwa mahakamani.
POLISI
KANDA MAALUM DSM WAMEKUSANYA TSH 414,060, 000 /= KUPITIA TOZO ZA MAKOSA YA
USALAMA BARABARANI
Jeshi
la Polisi Kanda maalum DSM kupitia Kikosi chake cha Usalama barabarani
kimekamata makosa mbalimbali ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia
tarehe 17.11.2016 hadi tarehe 21.11.2016 na kuingizia serikali mapato ya ndani
kama ifuatavyo;
1.
Idadi ya magari yaliyokamatwa - 12,923
|
2.
Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa - 879
|
3.
Daladala zilizokamatwa - 3,163
|
4.
Magari mengine (binafsi na malori)
- 9,760
|
5.
Bodaboda waliofikishwa
Mahakamani -
|
kwa makosa ya kutovaa helmet na
|
kupakia mishkaki -
|
6.
Jumla ya Makosa yaliyokamatwa - 13,802
|
Jumla
ya Fedha za Tozo zilizopatikana Tzs
414,060,000/=.
Madereva wote wanatakiwa kutii sheria
za usalama barabarani na washirikiane na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa juu
ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani ili kudhibiti matukio ya ajali
zinazoweza kuzuilika.
SIMON
N SIRRO- CP
KAMISHNA WA
POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment