Tuesday, November 8, 2016

YOUNG AFRICANS, RUVU SHOOTING SASA ALHAMISI


Wakati michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikifanyika kesho Jumatano Novemba 9, 2016, mchezo kati ya Young Africans na Ruvu Shooting utafanyika Alhamisi Novemba 10, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, imefahamika.

Mchezo huo umesogezwa mbele kwa siku moja kwa sababu Ruvu Shooting imechelewa kutoka Bukoba mkoani Kagera ambako Jumapili iliyopita ilicheza na Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limejiridhisha kuwa Ruvu Shooting imechelewa kuingia kituo cha Dar es Salaam, ndiyo maana mchezo dhidi ya Young Africans umesogezwa mbele.
Michezo mingine ya kesho Jumatano inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa Mwadui wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Mechi zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo.
Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.

No comments: