ACT WAZALENDO KUZINDUA KAMPENI ZAKE KESHO..NI UCHAGUZI MDOGO

TAARIFA KWA UMMA

KESHO Disemba 31/2016 Chama cha  ACT Wazalendo, tutazindua rasmi kampeni  za kuwania Ubunge na nafasi za udiwani katika kata ambazo tumesimamisha wagombea
Kutokana na uzinduzi huo awamu ya kwanza ya viongozi  wa kitaifa watagawanyika katika timu mbili tofauti  kwa ajili ya kushiriki kampeni hizo.

Timu ya kwanza itaongozwa na mwenyekiti wa Chama Mama Anna Mghwira na makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara, Mzee Shaban Mambo ambapo ziara yao itaanzia mkoani Geita katika kata ya Nkome(Disemba 31) Kahama katika kata ya Isagenhe(Januari Mosi),Dodoma katika kata ya Ihumwa(Januari 2),Morogoro, katika kata ya kiwanja cha ndege(Januari 3),Dar esSalaam katika kata ya Kijichi(Januari 4) na Zanzibar katika jimbo la Dimani (Januari 5)


Timu ya pili itaongozwa na kiongozi wa Chama Zitto Kabwe na Naibu katibu mkuu Bara Msafiri Mtemelwa, ambapo ziara yao itaanzia katika kata ya Kijichi jijini Dar esSalaam(Januari Mosi),Morogoro katika kata ya Kiwanja cha Ndege( Januari 2/2016) Ruvuma katika kata ya Tanga(Januari 3) Dodoma katika kata ya Ihumwa (Januari 4),Kahama katika kata ya Isagenhe(Januari 5) na Geita katika kata ya Nkome(Januari 6)
Chama cha ACT wazalendo kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika maeneo tuliyosimamisha wagombea wetu na kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kiuawajibikaji katika maeneo hayo huku tukitanguliza uzalendo kwa Taifa letu.

Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea kusisitiza kuwa pale ambapo chama hakijasimamisha mgombea, wanachama, wafuasi na wapenda demokrasia na mabadiliko ya kweli wahakikishe   wanampigia kura mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu katika eneo hilo.

Tunawahimiza wanachama wetu na wapenzi wa demokrasia popote pale walipo katika kata zinazofanyika uchaguzi kuhakikisha wanaiondoa CCM  kwa kuwachagua wagombea wa vyama vya upinzani kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao
Imetolewa na Abdallah Khamis
Afisa Habari ACT Wazalendo
30/12/2016

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.