JUMIA TRAVEL YAZINDUA KAMPENI YA PUNGUZO LA BEI KILA JUMATANO


JUMIA Travel yazindua kampeni ya punguzo la bei kila Jumatano

Baada ya kufanikiwa kwa kishindo kupitia kampeni yake ya ‘Black Friday’, kampuni inayoongoza kwa huduma za hoteli mtandaoni barani Afrika imekuja na ofa kabambe kwa wateja wake kila ifikapo siku ya Jumatano.

KUFUATIA mafanikio makubwa ya kampeni ya ‘Black Friday’ iliyovunja rekodi ya mauzo kwa zaidi ya 30% kwa siku, Jumia Travel imerudi tena na ofa kabambe inayokwenda kwa jina la ‘Travel Wednesday’ itakayokuwa ikifanyika kila siku ya Jumatano kupitia kwenye tovuti yake. Promosheni hii ambayo pia itajulikana kama “Dream Deals” inajumuisha punguzo kubwa la bei kwenye hoteli za hadhi ya juu ambazo zinazopendwa na watu wengi ikiwa ni muendelezo wa kuwapatia wateja machaguo mengi zaidi ya sehemu za kupumzika hususani kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.


Ingawa kampeni hii itaanza na idadi ya hoteli 5 ambazo zitakuwa zikitoa ofa kipindi cha promosheni, siku za usoni idadi itaongezeka na kufikia hoteli 12 ambapo ofa zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na Ijumaa. “Tumefanya hivi ili kuweza kuwaridhisha wateja wetu na kuwawezesha kuwa na machaguo ya huduma nafuu za kusafiri kupitia Jumia Travel. Kufuatia muitikio mkubwa wa kampeni ya ‘Black Friday’ kutoka kwa wateja wetu tumewaletea wapenda kusafiri wote ofa za aina yake tulizoingia makubaliano na maelfu ya hoteli barani Afrika,” alibainisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Travel, Bw. Paul Midy.

Ofa hizi tayari zimekwisha zinduliwa kwenye nchi kadhaa barani Afrika ambapo kampuni hii ni kinara katika utoaji wa huduma za malazi na usafiri ambazo wasafiri wengi wanaweza kuzimudu. Nchi hizo ni pamoja na Nigeria, Kenya, Uganda, Tanzania, Ivory Coast, Cameroon, Senegal, Ethiopia, Ghana, na Algeria.

Kama ilivyokuwa kwenye kampeni ya ‘Black Friday’, ofa hizi kabambe pia zitakuwa zikiendeshwa kwenye maeneo yote na nchi ambazo Jumia inafanya shughuli zake. “Zaidi ya 25% ya huduma za hoteli zilifanyika katika maeneo ambamo Jumia inapatikana. Hivyo basi, ni muhimu sana kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na kampuni zilizopo nchi zingine ili kuendelea kuvutia wateja wengi zaidi, kwani hili ndio lilikuwa dhumuni kubwa la kubadili muonekano wa kampuni hii,” alimalizia Bw. Midy.

Naye kwa upande wake Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania, Bi. Fatema Dharsee aliongezea kwa kusema kuwa, “Tunaamini kwamba kampeni ya ofa hii itakayokuwa ikifanyika kila siku ya Jumatano imekuja wakati muafaka ambapo watu wengi wa ndani na nje ya nchi wameshaanza au wanatarajia kuanza mapumziko kwa ajili ya msimu wa sikukuu. Kupitia ofa hizi mteja anaweza kujikuta analipia gharama nafuu za malazi katika hoteli za hadhi ya juu pasipo kutarajia, hivyo kujikuta anaokoa kiasi kikubwa cha fedha. Ningependa kuwasihi watu kutembelea kwenye tovuti pamoja na mitandao yetu ya kijamii ili kupata taarifa zaidi juu ya namna ya kufaidika na ofa hii.”

Wateja na watanzania kwa ujumla wanaweza kupata taarifa kuhusu kampeni hii kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii na tovuti ya Jumia Travel, majarida, ujumbe mfupi wa maneno na mingineyo.

Orodha ya hoteli zitakazokuwa zikitoa ofa hii ya punguzo la bei kila ifikapo siku ya Jumatano ni pamoja na Ngare Sero Mountain Lodge, Jangwani Sea Breeze Resort, Skippers Haven, na Golden Tulip Dar es Salaam.
Kuhusu Jumia Travel

Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ni kampuni nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika ambao humruhusu mteja kupata bei nzuri za hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote.

Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.

Hapa Jumia Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar Es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto (Ureno) na Paris (Ufaransa).

Kabla ya mwezi Juni mwaka 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mwaka 2013 na Jumia ambayo inaendeshwa kwa kushirikiana na MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axas.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.