Friday, December 30, 2016

MAPUNDA: ITC TAYARI TUMEIPATA

img_0122

Baada ya kususua kwa takribani majuma mawili sasa  hatimaye  hati ya uhamisho ya kiungo Mrisho Khalfan Ngassa imetua  kwenye klabu ya Mbeya City fc  asubuhi ya leo .

Akizungumza na mbeyacityfc.com muda mfupi uliopita Mwenyekiti wa City, Mussa Mapunda amethibitisha kutua kwa ITC hiyo kutoka shirikisho la soka la Oman ikiwa ni siku chache baada ya klabu ya Fanja  kumruhusu Mrisho Khalfan Ngassa kujiunga na kikosi cha City, ambayo pia  inajulikana  kama  timu ya kizazi kipya.
Ni kweli tumeipata, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa shirikisho la soka nchini,TFF, cham cha mpira cha Oman, hakika wamefanya kazi kubwa kufanikisha  kupatikana kwa ITC  hii na pia naishukuru Fanja Fc na watendaji wote kwenye timu yetu, tumekuwa na mawasiliano mazuri muda wote mpaka tumefanikiwa alisema.Akiendelea  zaidi, Mapunda alisema kuchelewa kufika kwa ITC hii hakukuwa na msuguano wowote baina ya vilabu hivi viwili kilichokuwa kinatokea  ni tofauti ya wakati na siku za ufanyaji kazi  kwenye ofisi kulingana  na taratibu za nchi hizi mbili.
Hakukuwa na msuguano wowote uliosababisha  kuchelewa kwa ITC  hii, kilichokuwepo ni utofauti wa taratibu za kiofisi  mara nyingi Oman siku za Ijumaa na jumamosi inakuwa ni mapumiko na huku kwetu Jumapili inakuwa mapumziko, hapo ndipo palikuwa panatuletea  mpishano, jambo jema ni kuwa tayari tumeipata na tunaweza kumtumia mchezaji kwenye michezo yote ya ligi na ingine ambayo inaihusu klabu yetu alisema.
Katika hatua nyingine Mapunda amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara   dhidi ya Mbao fc uliopangwa kuchezwa jumamosi kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa  yanaenda vizuri  huku imani kubwa kwa uongozi  wa City ikiwa ni kushinda mchezo huo hasa baada ya suluhu katika michezo miwili iliyopita.

No comments: