Thursday, December 22, 2016

POLISI WAMHOJI TUNDU LISSU KUHUSU NENO MTAKATIFU RAIS


TUNDULISU AHOJIWA KUHUSU "MTAKATIFU"...


1. Kwanza amehojiwa kwanini anamwita Mheshimiwa Bwana Mkubwa JPM kuwa ni Mtakatifu. Tundulisu amewashangaa Polisi kuwa kwa nini akiita lile jina linalohusiana na udikteta wanamfungulia kesi, Je na hili la Mtakatifu ni shida? Amehojiwa aeleze maana ya Mtakatifu akaeleza ni "asiye na hatia mbele ya Mungu na wanadamu".  

2. Kwanza amehojiwa kuhusu kikosi kazi kinachotesa watuhumiwa wanaokuwa chini ya polisi lakini huchukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha mateso na kurejeshwa alfajiri  Central Police.  Amewaambia Polisi kuwa yeye ameongea na walioteswa na wapo tayari kutoa ushahidi kuhusu ukatili wa kikosi kazi hicho. RCO wa Ilala amekana tuhuma za watuhumiwa kuteswa. 

3. Pili amehojiwa kuhusu sakata la kupotea Ben Saanane na polisi wanavyoweza kumtafuta amewaambia watafute mawasiliano yake ya mwisho waseme Saanane yuko wapi. 

#Note: Lissu amehojiwa chini ya usimamizi wa Wakili Fred Kiwhelo tangu saa Nne asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni hii. Polisi wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu maelezo hayo na Tundulisu ameachiwa.

Hii ni Kauli ya Tundu Lissu Baada ya Kutoka Polisi aliposhikiliwa kwa masaa kadhaa kwa mahojiano

Waheshimiwa nawasalimu kwa heshima zote. Muda mfupi uliopita nimetoka Kituo Kikùu cha Polisi, Central, Dar, nilikokuwa tangu asubuhi. Niliitwa kuhojiwa juu ya mambo mawili: kauli nilizotoa wakati wa press conference ya wiki iliyopita kwamba watu wanaomkosoa Mtakatifu Rais wetu mitandaoni wamekuwa wakikamatwa, kushikiliwa kwa muda mrefu bila kufikishwa kortini na kuteswa na kikosi kazi maalum kinacho-operate kutoka kwenye nyumba moja iliyoko Mikocheni, Dar.

 Polisi wanadai kauli hizo ni za kichochezi. Aidha wanadai kumwita Magufuli Mtakatifu Rais ni uchochezi mwingine. Sababu ya pili ya kuitwa Central ni kutoa taarifa za kusaidia polisi katika upelelezi wao kuhusu kupotea kwa Ben Saanane. Kuhusu uchochezi, nimewaeleza polisi kwamba ni kweli kuna kikundi maalum ambacho kinatesa watu wanaotuhumiwa kwa tuhuma za makosa ya mtandaoni na makosa ya ugaidi na ujangili. Ushahidi ni mkubwa sana juu ya suala hili. Walioteswa wapo na ndio waliotueleza mambo mabaya waliyofanyiwa.

Wengine niliwakuta mimi mwenyewe nilipokamatwa Juni mwaka huu na kulala Central wakati wa Uchochezi One. Kuhusu Mtakatifu Rais, nimewakumbusha kwamba nilipomwita Dikteta Uchwara walinikamata. Sasa nimemwita Mtakatifu Rais nayo shida,  inakuwaje??? Na by the way, tangu kesi ya Dikteta Uchwara One ilipoanza, mashahidi wao wameshindwa hata kuieleza Mahakama maana ya maneno 'Dikteta Uchwara.' In short, hakuna uchochezi wowote ambao nimefanya.

Ni mbinu zao tu za kutaka kutufunga midomo ili tusimseme huyu Mtakatifu wao anayedhani kinachotokwa kinywani mwake ndio sheria ya nchi. Kuhusu Ben Saanane, nimewaambia timu ya wapelelezi (hawa wako tofauti na walionihoji kuhusu uchochezi) kwamba kuna kila sababu ya kuamini kwamba kupotea kwa Ben Saanane kuna uhusiano na wale waliomtumia message kwamba 'his days are numbered' kwa kuendelea kwake kuhoji uhalali wa PhD ya Magufuli.

 Katika mazingira ya sasa ya kisiasa ambapo kila anayemsema Magufuli vibaya anakamatwa na kuteswa haiwezi kuwa ajabu kwamba Ben Saanane amepotea katika mazingira ya utata namna hii. Kitu muhimu hapa ni 'motive', nani atakuwa na sababu ya kumpoteza Ben Saanane. Walionihoji walikuwa 'very polite', lakini kilicho muhimu zaidi ni kwamba tuendelee kupaza sauti zetu serikali hii ituambie Ben yuko wapi. Hadi sasa hawajasema kama wamemkamata na/au wanamshikilia. Hawajasema kama ametoka nje ya nchi hii au la, na wao ndio wanaodhibiti exit points zote. Hawajasema mawasiliano yake ya mwisho yalikuwa lini, na nani, wapi na yalikuwa yanahusu nini. Wao ndio wana technical capabilities za kutuambia majibu ya maswali haya. Tuendelee kupiga kelele ili watoe actionable information kwa umma kuhusu Ben Saanane. Baada ya kuchukua maelezo kwa karibu masaa sita wameniachia kwa dhamana na wameahidi kuniita watakaponihitaji muda wowote. Niwatakieni Merry Christmas and Happy New Year 2017. Tundu

No comments: