SENTENSI 20 AMBAZO WANA CCM HAWATAZISAHAU KUTOKA KWA MWENYEKITI WAO MAGUFULI LEO


"Vyama vingine wakitaka kufanya vikao hapa Ikulu waombe ila tutataka kujua ajenda zao."


"Sioni aibu ya kuwakaribisha wanaCCM hapa Ikulu maana bila ninyi nisingefika hapa, hapa ni mahali pa watanzania wote'."

"Nitapenda chama changu CCM kizingatie kanuni za uchaguzi ikwemo kanuni ya kiongozi kuwa na nafasi moja tu ya uongozi."

"Nitapenda kuwa na jumuiya za chama zinazozingatia matakwa ya chama."

"Hii haitakuwa mara ya mwisho tutakapoamua hakuna mtu atakayenipangia nifanyie mkutano wapi."

"Hatutaki kuwa na chama legelege cha watu walalamikaji, sisi ndio tumepewa ridhaa na wananchi kuongoza."

"Napenda tuwe na chama kinachoongozwa na wanachama na sio chama kuongozwa na mtu chama ni mali ya wanachama na sio mtu."

"Nitapenda kuwa na jumuiya za chama zinazozingatia matakwa ya chama."

"Napenda tuwe na chama kinachoongozwa na wanachama na sio chama kuongozwa na mtu chama ni mali ya wanachama."

"Tunataka kununua meli mbili, moja ziwa Tanganyika na nyingine ziwa Victoria."

"Tunataka chama chetu kijitegemee kiuchumi, ni aibu kutegemea fedha za ruzuku na watu binafsi ili kujiendesha."

"Rasimali nyingi hatunufaiki nazo kutokana na mikataba isiyo na tija, usimamizi mbovu na ubadhirifu."

"Wapo wananchama wachache ambao ukisaliti chama chetu hasa kipindi cha uchaguzi na wengine kuendeleza makundi."

"Katika awamu hii hatutamsamehe mtu yeyote wa kutafuta uongozi kwa njia ya rushwa."

"Naziagiza jumuiya zote kuhakikisha kanuni zao zinaendana na katiba ya C.C.M......"

"CCM itaongeza idadi ya Wanachama, kupambana dhidi ya Rushwa, kujitegemea Kiuchumi, kukomesha makundi ndani ya Chama, kujiimarisha ngazi ya chini ya Wanachama".

"Napenda kuona sasa  mtu mmoja akishika cheo kimoja ndani ya C.C.M badala ya vyeo vingi kama ilivyo sasa"

"CCM kuzingatia Kanuni zake za uchaguzi, Kanuni za Jumuiya ziendane na Katiba ya Chama, CCM kuongozwa na wanachama badala ya chama kuongozwa na Mwanachama".

"Nitapenda sana chini ya uongozi wangu, vikao vya maamuzi huku juu viwe na watu wachache."

"Nawaomba wajumbe mabadiliko yatakayoletwa kwenu myachambue, myapitie na kisha kuyapitisha kwa maslahi ya chama chetu CCM maana sisi Kamati Kuu tumeshayapitisha sio kwa vyeo vyetu bali maslahi ya chama chetu."

Dk.John P. Magufuli
Mwenyekiti CCM Taifa.

Ufunguzi Kikao cha NEC 13/12/2016

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.