Saturday, December 10, 2016

Tizama maadhimisho ya siku ya akimataifa ya Haki za binadamu ilivyoadhimishwa na LHRC Jijini Da es salaam


Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Hellen Kijo Bisimba , akiwa na  Balozi wa uingereza nchini Tanzania  mh Sarah Cooke wakiwa katika  maadhimisho ya siku ya haki za binadamu yaliyofanyika Makumbusho Jijini Dar es salaam Jana.Picha na Exaud Mtei











Mgeni Rasmi ambaye ni Balozi wa uingereza nchini Tanzania  mh Sarah Cooke akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika Jijini Dar es salaam na kuadhimishwa na kituo cha sheria na hakii za Binadamu nchini.
Picha Ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo

Viongozi mbalimbali wa Club za LHRC kutoka mashule na Vyuo mbalimbali nchini wakishiriki kwa pamoja kuzindua Report mpya ya hali za Haki za binadamu nchini Report ambayo imeandaliwa na Kituo cha sheria na Haki za binadamu nchini Tanzania LHRC 

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu bi Hellen Kijo Bisimba akizungumza na wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu na wanafunzi  waliojitokeza katika Maadhimisho hayo yaliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Report Mpya ya haki za binadamu nchini

Wanafunzi wakisikiliza kwa makini
Kutokana na utafiti uliofanywa na kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania kwa mwaka 2016 imeonekana kuwa na ukandamizaji wa haki ya Uhuru kukusanyika kutokana na katazo la kuto kufanya Mikutano ya kisiasa hadi itakapofika mwaka 2020.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu ulimwenguni yaliyo fanyika Leo hii katika Makumbusho ya Taifa Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Dr.Helen Bisimba amesema ripoti hiyo ya mtazamo imejikita katika maswala 6 ya haki za kiraia na kisiasa.

  Bisimba amesema maswala hayo ni pamoja na uhuru wa kujieleza haki ya kupiga kura,uhuru wa kukusanyika,haki ya kuishi kwa upande wa mauaji na ukatili mikononimwa vyombo vya Dola, kujichukulia sheria mkononi NA mauaji yanayotokana na amani za kishirikina.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameipongeza serikali kwa kufanya mabadiliko ya msingi katika kupunguza rushwa na ubadhilifu serikalini japo kuwa bado kuna ukandamizwaji unaotokana na sheria mpya zinazoleta vikwazo vipya kwenye haki ya kujieleza na mchakato wa utungaji wa sheria Huduma za vyombo vya habari.

Ikumbukwe kwamba kila tareh,10 ya Mwezi huu wa 12 kila mwaka tangu mwaka 1950 imekuwa ni siku maalumu ya haki za binadamu kimataifa, na tangu kusajiliwa kwa kituo hiki mwaka 1995 wamekua wakiadhimisha siku hii kwa kufanya shughuli mbali mbali ili kuinua juu ajenda ya haki za binadamu.


No comments: