Sunday, December 18, 2016

WATAALAM WATOKA NA MAPENDEKEZO KADHAA KUHUSU SHERIA YA NDOA NCHINI TANZANIA

 Wakati nchini Tanzania wanasheria pamoja na wadau mbalimbali wa maswala ya sheria wakeiendelea kuishawishi serikali hiyo kuifanyia marekebisho sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ya nchini Tanzania hatimaye Wizara ya Katiba na sharia kwa kushirikiana na mashirika ya  Action Aid na TGNP wamewakutanisha wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia,wanazuoni na wanahabari na kuwapa nafasi ya kupitia sheria hiyo na kupendekeza baadhi ya marekebisho ambayo wanadhani yanastahili kufanyika katika sheria hiyo.
Sheria ya Ndoa nchini Tanzania ni moja kati ya sheria ambazo zimekuwa zikizua gumzo kwa kipindi kirefu hadi kufikia hatua ya baadhi ya wanaharakati kufungua kesi mahakamani kupinga baadhi ya vifungu ambavyo wanadai vimekuwa vikikinzana na sharia nyingine ziliozopo nchini.


Katika mkutano mapitio ya sheria hiyo ambao umemalizika Jijini Dar es salaam na  kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria kutoka maeneo mbalalimbali,wadau kutoka katika asasi za kiraia,wanahabari na pia kuhudhuriwa na wadau wakubwa wa sheria hiyo kutoka wizara ya katiba na sheria wametumia muda mwingi kuipitia sharia hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maoni na maoendekezo yao.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu mwakilishi kutoka serikalini aliyekuwa katika kikao hicho Bwana Cazmiry Sabath alisema kuwa lengo kuu la kuwakutanisha wadau hao ni kuchukua maoni ya jinsi gani ya kutekebisha na kuifanya sheria ya ndoa nchini Tanzania kuwa bora Zaidi tofauti na sasa ambapo imekuwa ikilalamikiwa na wadau mbalimbali huku akisema ni mwendelezo wa kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii kusikia wanasema nini juu ya sheria hiyo

Baadhi ya vifungu ambavyo vilijadiliwa kwa kina na kuonekana vinahitaji marekebisho ni pamoja na kifungu cha 69-71 kinachozngumzia kuhusu mtu kuwa na uwezo wa kumshtaki mwenzake ambaye aliahidi kumuoa na baadae kuvunja ahadi hiyo ambapo wadaun hao walitoa mapendekezo kadhaa huku wengine wakitaka kifungu hicho kiweke wazi ni lini ahadi ya ndoa inaanza kuhesabiwa,Kifungu cha 72 ambacho kinamtaka mtu akikamatwa Ugoni alipe faini ya shilingi laki mbili ambapo wadau hao walidai kuwa faini hiyo ni udhalilishaji kwa kuwa wapo watu wenye uwezo wa kulipa hivyo hiyo sio dawa ya kupunguza matukio hayo bali ni kuyaongeza Zaidi.
Sheria ya ndoa imekuwa ikizua gumzo hasa katika kifungu kinachozungumzia umri wa mtu kuolewa ambapo kimekuwa kikikinzana na sheria ya mtoto ambayo inamtaja mtoto kuwa ni mtu mwenye umri wa miaka 18 kushuka chini huku sheria ya ndoa ikisema mtu anaweza kuolewa hadi na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi jambo ambalo wanaharakati mbalimbali wapo mahakamani kutetea sakata hilo.

Katika mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya katiba na sheria kwa kushirikiana na  Mtandao wa TGNP na USAID wasomi mbalimbali walitoa maoni yao akiwemo Cazmiry Sabath kutoka Serikalini,Scholastica Haule, kutoka Action Aid Tz,Dr Hashir Twaibu Abdallah( kutoka kitivo cha sharia UDSM) Mhadhiri na mwanasheria. Richard Mbonde huyu ndiye mwenyekiti wa kikao na Bwana Michael Mushi, ambaye ni wakili kutoka kampuni ya ushauri wa miradi iliyopo shekilango .

No comments: