HUU NDIO UJUMBE WALIOTUMA WACHIMBAJI WALIOFUKIWA NA KIFUSI GEITA,WADAI WAPO HAI,WATAKA CHAKULA NA SIGARA

Wakati imeelezwa kuwa waokoaji katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko Geita , wamebakiza mita tatu kuwafikia waliofukiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani akizungumza na ndugu wa watu waliofukiwa amesema kwamba wanafanya mpango wa kuwapelekea chakula wachimbaji hao.

Amesema kwamba jana wamefanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na kwamba wapo kumi na watano na kuwa wanachohitaji kwa sasa ni chakula.


Alisema waokoaji walifanikiwa kuwafikishia kamba na kalamu watu hao ambao waliandika majina na mahitaji yao na kusema kwamba wote wapo salama.


Watu hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya uokoaji.

Watu wengi wapo katika eneo hilo wakiwemo ndugu wa waliofukiwa lakini kwa juhudi wanazoziona za uokoaji wametulia na kufuata maelekezo wanayopewa ikiwemo kukaa mita 500 toka eneo la tukio.
Soma hapa ujumbe waliotuma
CHANZO MALUNDE1 BLOG

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.