Tuesday, January 3, 2017

ZITTO KABWE:UHABA WA CHAKULA NI KIBURI CHA SERIKALI

 HOTUBA YA KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT Wazalendo NDG ZITTO KABWE KATIKA KATA YA KIWANJA NDEBELE MANISPAA YA MOROGORO JANUARI 2/2017
Hali ya chakula nchini sio nzuri. Wananchi mmeshuhudia namna bei za vyakula zinapanda kila siku. bei ya sembe sasa kilo moja imefikia tshs 1600 hapa morogoro. Mchele kilo tshs 1500, maana yake leo ugali na wali imekuwa bei inafanana. Gharama za maisha zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa.

Kwanini hali ya chakula inazidi kuwa mbaya? ni kwa sababu ya maamuzi mabovu ya Serikali kuhusu hifadhi ya chakula. Serikali zote zilizopita huko nyuma zilikuwa zinanunua chakula cha akiba ili wakati wa ukame kama sasa chakula hicho kiingie Sokoni na hivyo kushusha bei na kuwezesha wananchi kumudu gharama za chakula.

 Rais wetu kawaambia wananchi wa Kagera kwamba Serikali haina shamba hivyo hakuna chakula cha njaa,hii kauli sio ya uongozi. ni kauli ya kuficha maamuzi ya serikali yaliyotupelekea kukosa akiba ya chakula.

Wananchi, leo tunavyoongea ghala la chakula la Taifa lina tani 90,000 tu za chakula. Kipindi Kama hiki mwaka 2015 ghala la chakula lilikuwa na tani 450,000. Chakula kilichopo kwenye ghala kinatosha kwa wiki moja tu. Takwimu hizi zote zipo kwenye Taarifa ya Benki Kuu ya Mapitio ya uchumi ya mwezi Novemba.

Serikali ya awamu ya tano iliamua kutonunua chakula kuweka kwenye ghala la Taifa kwa kisingizio cha kubana matumizi. Sasa Hali ya chakula imekuwa mbaya Rais anasema ' kila mtu atabeba msalaba wake Mwenyewe '. Sio sahihi. njaa ya sasa sio sababu ya ukame tu, ni sababu ya maamuzi mabovu ya Serikali.

Wananchi wa Morogoro, kuna njia moja tu ya kuikumbusha Serikali kutekeleza wajibu wake. ni kuwanyima kura kwenye uchaguzi huu. Tukiwanyima udiwani kwenye kata watajiuliza kunani. Watapata majibu kuwa hamtaki njaa na mnaitaka serikali ichukue hatua badala ya kukimbia majukumu yao na kusema kila mtu atabeba msalaba wake Mwenyewe.

Chaguzi hizi ndogo ni fursa ya kuonyesha kutorodhishwa kwetu na uendeshaji wa uchumi wa nchi yetu. Wananchi wa kata ya Kiwanja cha Ndege hapa morogoro tumieni fursa hii kwa kupiga kura kuchagua diwani kutoka cha cha ACT Wazalendo
Vyama vya siasa vimekuwa haviwezi kufanya mikutano namna hii kuanzia mwaka jana  kwa kuwa Rais ameamua mpaka 2020, ameshindwa kutambua kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya kikatabia

Jambo moja alilosahau Rais katika katazo lake la mikutano  ni kuwa kuna mpangaji Mwenye mamlaka zaidi yake naye ni Mwenyezi Mungu,hivyo anapotoa amri zake ajue kuwa kuna Mungu ambaye naye ana mipango yake  na ndiyo kama hii inayotufanya leo tuwahutubie katika mikutano ya hadhara.

Uchaguzi Wa marudio katika kata na jimbo unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo  umekuwa ni jaribio la wazi Kwa Rais juu ya kuheshimu katiba kama na hili angeweza kuzuia
Kuhusu mgombea udiwani Wa ACT katika kata ya Kiwanja cha ndege,Zitto alisema matokeo yoyote hayataenda kubadili mfumo Wa Uongozi ndani ya baraza bali kuhimiza uadilifu na kwamba vyama vilivyo ndani ya baraza kwa sasa haviwezi kusemana zaidi ya kufichiana uovu

Amesisitiza kuwa wananchi wakimchagua mgombea Wa ACT Wazalendo ataenda kuwa mwangalizi Wa maovu yote yaliyoshindwa kusimamiwa ndani ya manispaa ya Morogoro.
Alisema kama watampa nafasi Mgombea Wa ACT Wazalendo Rahim Elias ataenda kuwa mwiba ndani ya manispaa na kuhakikisha vijana na kina mama katika manispaa hiyo wananufaika kwa ile asilimia kumi inayopaswa kutengwa kisheria.


 Alisema upinzani Wa kweli ni lazima uoneshe utofauti Wa kiuongozi na CCM na badala yake ufanye vile vitu wananchi wanavitaka
"Hatuji kuwaahidi mbingu wala asali na maziwa bali tunawaahidi Uongozi ulio bora na kikubwa tupeni kata hii ya Kiwanja cha ndege iwe mfano Wa maeneo mengine kwa siku zijazo"


 Aisema kwa sasa kuna tatizo kubwa la uendeshaji Wa nchi licha ya hatua kubwa ya kupambana na ubadhirifu na ufisadi lakini maisha ya wananchi yamesahaulika
Rais anapochukua hatua ya kupambana na ufisadi na kusahau maisha ya wananchi kwa kigezo cha kuwa anaionyoosha nchi  hili ni tatizo,ni vema ajue hatumpingi katika kupambana na ufisadi na tupo pamoja nae lakini hatutasita kumkosoa pale anapokosea hasa tunapoona maisha ya wananchi hayapewi kipaumbele
Tatizo viongozi wa  safari hii wamesahau  kuwekeza nguvu katika kusimamia matatizo ya wananchi wao wakajielekeza katika kutumbua majipu utafikiri wananchi watashiba majipu


 Leo hii ninapoongea na ninyi kwa takwimu za Jana chakula cha akiba kilichopo kinatosha kwa siku nane tu na Rais leo amesema hakuna wilaya itakayopelekewa chakula lakini amesahau kwamba wajibu Wa serikali ni kuhakiksha chakula cha akiba kinakuwepo na akumbuke hata watangulizi wake hawakuwa na mashamba ya serikali bali walikuwa wananunua na kuhifadhi lakini sasa hivi Rais kakataa kununua chakula


 Mkitaka kumjaza Sifa Rais aendelee kutumbua majipu na kusahau kusimamia shida za wananchi basi mpeni diwani wa ziada na mkitaka kumstua basi mnyimeni diwani na kuwapa wapinzani ili ajue kuwa kuna mambo anaharibu


 Kata zingine pamoja na hii zina fursa ya kumtumia Rais salam kuwa kuna mambo hayaendi sawa hatuwezi kuwa tunatumbua majipu Mwaka mzima bila kusimamia shida za wananchi


No comments: